Kufafanua Changamoto za kuwa Mama kwa Neema

22 September 2026

Kufafanua Changamoto za kuwa Mama kwa Neema

22 September 2026

Ukomavu wa Kikristo ni nini?

Bustani yetu ina mti mdogo wa tufaha. Kila mwaka hukua kidogo, na matunda yake huzidi kuwa mengi. Umekomaa kadiri miaka inavyoongezeka, na imekuwa baraka kunufaika na matunda ya ukomavu huo.

Kwa namna nyingi, hii ni taswira ya kile ambacho maisha ya Kikristo yanatuitia—ukuaji unaozidi kuongezeka wenye matunda. Hivyo twasoma, “Kwa hiyo … tukisonga mbele ili tufikie utimilifu” (Waebrania 6:1).”

 Mfano wa Ukomavu 

Tumeonyeshwa ukomavu wa Kikristo katika Bwana Yesu. Ni kwa kukubaliana naye ndipo tunapokomaa na kuzaa matunda.

Kuna mwelekeo wa kupunguza uhalisia wa maisha ya kibinadamu ya Bwana Yesu Kristo. Lakini kulikuwa na Ukuaji wa kweli katika ukomavu kwenye maisha ya Kristo. Alikuwa mkamilifu akiwa mchanga, mtoto, na mtu mzima. Alikomaa bila dhambi akipitia kila moja ya hatua hizi.

Tunaambiwa hivi katika Luka 2:40:”Naye yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu, akijawa na hekima. Na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. Kama Calvin anavyoeleza, “Kristo alifanyika mwanadamu halisi… kwa hiari alijitwika kila kitu kisichoweza kutenganishwa na asili ya mwanadamu” Hilo linajumuisha kukomaa.

Kristo alikomaa kadiri alivyofundishwa Neno na Baba yake: 

Huniamsha asubuhi kwa asubuhi ;

 Huamsha sikio langu 

lisikie; kama afundishwaye.(Isaya 50:4)

Pia alikomaa kupitia majaribu na mateso ya maisha katika ulimwengu ulioanguka. Mwandishi wa Waebrania asema, “Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utiifu kutokana na mateso aliyoyapata” (Waebrania. 5:8). Katika kila hatua, utiifu wa Yesu ulikuwa mkamilifu, lakini mateso Yake yalimwongoza kwenye utiifu na ukomavu unaozidi kuongezeka daima.

Njia ya Ukomavu 

Kristo si tu mfano wa ukomavu; Yeye ndiye njia ya ukomavu wa Kikristo. Tunda linaweza kukua tu linapounganishwa na mti. John Brown wa Wamphray anasema,

“Hakuna kushiriki katika aina yoyote ya mvuto wa kiroho unaotoka kwa Bwana Yesu, ambao kwa huo maovu yanaweza kudhalilishwa na mtu mpya akaanza kukua, mpaka tunapounganishwa na Kristo na kufanywa kuwa mmoja naye kwa imani.”

Ukomavu hukua “ndani Yake.”

Ukomavu huu hukua kwa kutumia njia alizoziweka Kristo. Paulo asema katika Waefeso 4 kwamba Yesu amelipa kanisa karama “wachungaji na walimu,” nao wamepewa ili kutuleta “kuwa watu wazima, kwa kufikia kimo cha ukamilifu wa Kristo.” (Waefeso 4:11, 13). Ili kufaidika na wachungaji ambao Mungu amelipa kanisa lake, “Basi hatutakuwa tena watoto wachanga, tukiyumbishwa na mawimbi, na tukipeperushwa hapa na pale na kila upepo wa mafundisho… badala yake, tukiambiana kweli kwa upendo, katika mambo yote tukue, hata tumfikie yeye aliye kichwa, yaani Kristo” (Waefeso 4:14, 15). Kusikiliza na kushikilia mafundisho ya Neno huleta uthabiti wa kiimani na hutulinda tusipotoshwe na mafundisho ya uongo.Hii inatufanya tuzidi kufanana na Kristo, aliye kichwa chetu. Huu ndio ukomavu. Kuona ukomavu huu kwa wasikilizaji wao ndilo lengo la wahubiri: “Yeye ndiye tunayemtangaza, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja akiwa amekamilika katika Kristo” (Wakolosai 1:28).

Ukomavu wa kufanana na Kristo pia hutokana na kupitia mateso ulimwenguni. Warumi 5:3–4 inasema, “Si hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi,nayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini.” Majaribu na dhiki za maisha katika ulimwengu ulioanguka hukuza tabia zetu zinazofanana na Kristo.

Tunapobarikiwa kwa mafundisho ya Neno, tunapotakaswa kwa kupitia majaribu ya maisha, kutakuwa na kukomaa. Kitabu cha Mithali kinasema, “Mfundishe mtu mwenye hekima naye atakuwa na hekima zaidi”(Mithali 9:9). Tumeambiwa pia kwamba mateso “huzaa matunda ya haki na amani kwa wale waliofunzwa nayo” (Waebrania 12:11).

Ushahidi wa Kutokomaa Kiroho

Ukomavu ni kufanana na Kristo. Lakini tunaweza pia kuona kinyume cha ukomavu —kutokomaa. Tuna maelezo marefu ya kutokomaa katika Waebrania 5:12–14: Tunaambiwa kwamba waamini walikuwa hawajui. ”hatua za awali za kweli za neno la Mungu. Mnahitaji maziwa, wala si chakula kigumu,” hawakujizoeza “kupambanua kati ya mema na mabaya.” (Waebrania 5:12–14). Maziwa na uchanga wa kiroho vina wakati wake na mahali pake (1Petro 2:2; 1 Wakorintho 13:11). Lakini Wakristo hawakusudiwi kubaki katika ujinga wa mafundisho ,au kutokuwa na msimamo thabiti wa kimaadili wa kutofautisha mema na mabaya. La, ukomavu wa Kikristo ni kinyume cha mambo haya.

Dalili nyingine ya kutokomaa kiroho imewekwa wazi katika 1 Wakorintho 3:1–3: Paulo anawaandikia Wakorintho kama “watoto wachanga katika Kristo,” akisema ”kuna wivu na magombano miongoni mwenu. ” (1 Wakorintho 3:1–3). Migawanyiko ya kanisa juu ya watu fulani hufichua uchanga wa kiroho. Ukomavu wa Kikristo, kwa upande mwingine, ni upendo wa umoja miongoni mwa waamini.

Hitimisho

Wakristo hawatafikia ukomavu mkamilifu katika maisha haya. Ukuaji unahitajika kila wakati. Tumeitwa kukua ”Bali kueni katika neema na katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo” (2 Petro 3:18). Ukomavu wetu kamili utatimia mbinguni. Ni pale tutakapomwona Yeye ndipo tutatafanana Naye (1 Yohana 3:2) (1 Yohana 3:2). Siku hiyo tu ndipo utukufu wote wa ukomavu utakuwa wetu. Kwa sasa, sisi , Nasi ”tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, unaotoka kwa Bwana, aliye Roho” (2 Wakorintho 3:18).

Siku ya kufikia ukomavu kamili wa kufanana na Kristo ni hakika: ”pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa Mwanawe(Warumi 8:29). Tutakomaa katika Kristo. Ni tumaini la ajabu!


Makala haya yalichapishwa awali kwenye Blogu ya Ligonier Ministries.

Donald MacLean

Donald MacLean

Dkt. Donald John MacLean ni rais wa Westminster Seminary UK ambako pia hutumika kama profesa wa theolojia ya kihistoria na ya mfumo. Yeye ni mhariri wa Foundations, jarida la kitheolojia la Affinity, na pia hutumika kama mdhamini wa Banner of Truth na wa Tyndale House, Cambridge.