Theolojia ya Agano kwa Watoto: Mwongozo wa Wanafunzi

6 October 2026

Theolojia ya Agano kwa Watoto: Mwongozo wa Wanafunzi

6 October 2026

Njia za Baba katika Nyakati Ngumu

Kuwa baba kumejaa changamoto. Miongoni mwa mambo magumu zaidi ni kumwangalia mtoto wa kiume au wa kike aliyepotoka—ijapokuwa alilelewa katika familia ya Kristo —akiiacha imani. Tugeukie nini?

Kitabu cha Mithali hutia moyo na hutoa ufahamu wa kuelekeza njia ya kupita katika maji hayo yenye hatari. Iliandikwa kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.

huwapa busara wajinga,

maarifa na akili kwa vijana—

wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,

wenye kupambanua na wapate mwongozo(Mitahli 1:4-5)

Tumaini la baba kuhusu ustawi wa mtoto wake huwasilishwa kwanza kupitia mafundisho ya kumcha Mungu. Sura za kwanza za Mithali zinawasihi watoto wa kiume na wakike “sikiliza mwongozo wa baba yako” (Mithali 1:8); “utayakubali maneno yangu” (Mithali 2:1); “usisahau mafundisho yangu” (Mithali 3:1);“Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba” (Mithali 4:1); “sikiliza kwa makini hekima yangu” (Mithali 5:1); “fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru,” (Mithali 6:3); na “shika maneno yanguna kuzihifadhi amri zangu ndani yako” (Mithali 7:1). Je, tumefanya kile tulichoweza kuwafundisha  ukweli wa Biblia katika mioyo na akili zao?

Kinababa wanapaswa pia kuchunguza kwa makini mwenendo wa mwana mpotevu. Mithali inaainisha hali tatu hatari za moyo: mjinga anayemsahau Mungu, mwenye dhihaka anayempuzia Mungu, na mpumbavu anayemkataa Mungu (Mithali 1:22). Kila hatua huzidisha ugumu wa moyo, kutoruhusu kweli za kiroho, na kuwa karibu zaidi na hatari. Ufunguo ni kubaini sauti zipi wanazozisikiliza kwa makini zaidi. Hutembea, husimama, au huketi na kina nani?

 Mjinga ni mtu asiye na uzoefu; husikiliza sauti za majaribu na hushawishika kwa urahisi na marafiki wabaya. Hekima inapaza sauti kwa mjinga aone mwisho wa chaguo lake na aachane na desturi au marafiki hao (Mithali 7:6–27). Mwenye dhihaka ni mwenye kiburi zaidi; hudhihaki dhambi na hupuuza kila shauri la kimungu. Hekima humtia changamoto mtu kusikiliza karipio la baba yake, asije akaangukia uharibifu, aibu, na fedheha (Mithali 13:1). Mpumbavu humkataa Mungu kwa ukaidi na hulidharau Neno Lake. Hekima humwonya mtu wa namna hii kwamba kwa kujifanya kiziwi hujiletea maangamizi, na mwisho wake ni njia ya mauti. Omba hekima ili ujue jinsi (na mara ngapi) ya kusema ukweli katika upendo.

Ni hatua gani nyingine za vitendo ambazo akina baba wanahimizwa kuzifuata?

Sala

Nyenzo ya kwanza na ya juu kabisa ya baba ni kumleta mtoto kwa kudumu mbele ya kiti cha enzi cha neema. John Yates, mchungaji mwenye uzoefu na baba wa watoto na wajukuu wengi, anaandika kutokana na tajiriba: “Kwa haraka sana, watoto huanza kumfundisha mtu kuhusu upungufu wake mwenyewe, kwamba hana majibu yote, na kwamba mara kwa mara anashindwa kama mume na baba. . . . Huu ndio mwanzo wa njia mpya kabisa ya maisha iitwayo sala.”1 Yates anapendekeza nyenzo yenye msaada mkubwa—kijitabu cha maombi cha kufuatilia mahitaji mahususi na majibu kwa kila mwanafamilia. Maombi ya baba ya kudumu yana faida nyingi.

Toba

Kiungo kilichovunjika katika safari ya kiroho wa mtoto aliyepotea au anayerudi nyuma kinaweza kuwa kosa la baba. Je, tumewaambia hivi karibuni jinsi tunavyowapenda? Je, tumekiri kwa unyenyekevu mbele yao dhambi zetu wenyewe kama baba? Hujachelewa kamwe kuomba msamaha wa kweli kwa maneno ya hasira au ya kuumiza, au kwa adhabu iliyokuwa legevu, isiyo thabiti, au iliyokuwa kali kupita kiasi. Wanaume wa kweli huchukua hatua ya kwanza ya kuomba msamaha.

Usikate tamaa. Baba mwenye hekima huendelea kwa uthabiti kutafuta uhusiano wa kweli kwa kadiri mwana mpotevu anavyoruhusu.

Maungamo yoyote ni vyema zaidi yakitolewa uso kwa uso, ingawa mazungumzo ya mtandaoni, simu, au taarifa iliyoandikwa (kwa mpangilio unaopungua) yanaweza kuwa muhimu. Taarifa hiyo inapaswa kuandikwa kwa mkono, kwa kuwa barua za kibinafsi kutoka mkononi mwako zina uzito mkubwa kuliko barua pepe au ujumbe mfupi.

Uvumilivu

Mchungaji mmoja aliandika kitabu chenye maono ya ndani mwaka 1876 kuhusu familia ya Kikristo. Ndani yake, anawasihi akina baba waongoze kundi lao kwa uvumilivu: “Lengo si kuvunja moyo , bali kuuelimisha; si kuufunga uhuru wake kwa nguvu za nje, bali kuufundisha kujidhibiti.”2 Toeni nafasi kwa kazi ya neema, ambayo mara nyingi huwa ya polepole, kuzuia kilicho hayawani, mkiteka moyo wa mtoto si kwa shambulio bali kwa ushawishi wa taratibu.

Upole

Kwa sasa, usiwe mkorofi na mgomvi. Sema ukweli kwa uwazi, lakini sio kila mara unapozungumza. Tumia maneno (yaliyopangwa mapema) yanayoonyesha upendo,sio hasira; uvumilivu, siyo kuchanganyikiwa. “Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana” (Efe 6:4). Dumisha uhusiano kwa kufanya shughuli za kufurahisha pamoja kadiri inavyowezekana. Muombe Bwana akupe moyo wa kukaribisha na mbinu za ubunifu za kujenga mahusiano mapya, ukipata furaha katika shughuli za pamoja.

Ustahimilivu

Usikate tamaa. Baba mwenye hekima huendelea kwa uthabiti kutafuta uhusiano wa kweli kwa kadiri mwana mpotevu anavyoruhusu. Upendo usio na masharti husema, “Nakupenda bila kujali ulichokifanya.” Kielelezo kizuri zaidi kinapatikana katika mfano wa Kristo kuhusu mwana mpotevu. Baba aliyekataliwa aliendelea kuwa macho kila wakati akimsubiri mwanawe aliyepotea, akiangalia upeo wa macho kila siku akitarajia kurudi kwake. Alipomuona kijana akichecheme akirudi nyumbani, alijawa na huruma, akakimbia kumkumbatia. Akamsamehe buharibifu wake wa anasa na akamrejesha kikamilifu nyumbani mwao, “Wakaanza kusherekea” (Luka 15:24) Wajulishe kwamba daima utaacha taa linalowaka.

Hatimaye, akina baba, jiwekeni ninyi pamoja na watoto wenu mikononi mwa Bwana. Ukombozi mwishowe ni kazi yake peke yake, wala mkono wake si mfupi hata usiweze kuokoa.

John W. Yates II, How A Man Prays for His Family (FamilyLife Publishing, 2020), 9. ↩

B.M. Palmer, The Family in Its Civil and Churchly Aspects (Sprinkle Publications, 1991), 82. ↩

  1. John W. Yates II, How A Man Prays for His Family (FamilyLife Publishing, 2020), 9. ↩
  1. B.M. Palmer, The Family in Its Civil and Churchly Aspects (Sprinkle Publications, 1991), 82. ↩

Makala haya yalichapishwa awali kwenye Blogu ya Ligonier Ministries.

Kenneth Wingate

Kenneth Wingate

Kenneth B. Wingate ni mwanasheria huko Columbia, S.C., na ni mzee Kiongozi katika First Presbyterian Church. Yeye ndiye mwandishi wa A Father’s Gift: Lessons from Proverbs na Rich Grace in Poor Soil: Growing in the Master’s Grip.