
Ghadhabu ya Mungu ni nini?
25 June 2026
Wajibu wa Tumaini katika Maisha ya Kikristo
2 July 2026Kutatua Hatia ya Utoaji Mimba
Maelfu ya watu wanasumbuka na hatia inayohusiana na utoaji mimba. Inawasumbua wanawake ambao wamewahi kutoa mimba, wanaume ambao wamewahimiza, na madaktari ambao wamewafanyia. Daktari mmoja alitangaza katika The New York Times kwamba alilazimika kujiandaa kihisia na mara nyingi alikosa usingizi kabla ya kufanya utoaji mimba: “Ni jambo gumu sana kwa daktari wa wanawake kulifanya,” alisema. “Hisia zinazosababishwa ni kali sana . . .kiasi kwamba madaktari hawazizungumzii kati yao.” Katika tukio moja, daktari huyu alianguka sakafuni, akizidiwa na hisia, baada ya kufanya utoaji mimba.
Hatia ni hisia yenye nguvu, ambayo ina uwezo wa kuwasababishia watu kupooza kisaikolojia vibaya sana. Wakati mmoja niliongeleshwa na daktari anayefanya kazi na magonjwa ya akili na alinipa fursa ya kujiunga na wafanyakazi wake. Alieleza kwamba idadi kubwa ya wagonjwa wake walikuwa wakisumbuliwa na matatizo yanayohusiana na hatia mbaya. “Hawa watu hawahitaji daktari, wanamhitaji mchungji,” alisema. “Wanahitaji mtu wa kuwaambia kwamba wamesamehewa.”
Mtaalamu huyu wa magonjwa ya akili hakuwa mwaminifu kwa Ukristo; alijali tu kuhusu afya ya akili ya wagonjwa wake. Alielewa nguvu inayoharibu ya hatia isiyosuluhishwa, na alitambua kwamba kukana na kuirazinisha havikuwa njia bora za kushughulikia hatia halisi. Dawa pekee inayofanyakazi kwa hatia halisi ni msamaha wa kweli. Kujaribu kufunika doa mikononi mwetu ni mbadala duni wa kuondoa doa hilo.
Kuhisi msamaha wa Mungu
Ili kupata uhuru wa kina wa msamaha, mtu lazima amwendee Mungu na kukiri dhambi kwa moyo mnyenyekevu na kuwa na roho iliyovunjika. Moyo ulipondeka unahusisha huzuni ya kweli na ya kimungu kwa kutomtii Mungu. Inatofautiana na toba ya hofu, ambayo ni aina ya uongo ya toba inayochochewa na hofu ya adhabu. Majuto yanaonekana kwa mtoto ambaye, anapoona kiboko mkononi mwa mama yake, anajutia kwamba alikamatwa akiwa anachukua biskuiti. Toba ya kweli inakubali ukweli wa hatia na haijaribu kujihesabia haki.. Yeyote anayemwendea Mungu kwa unyenyekevu wa kweli, kupondeka, na azimio la dhati la kutotenda dhambi tena atapokea msamaha wa Mungu bila shaka…
Ingawa kile nilichokifanya hakiwezi kubadilishwa, naweza kusamehewa. Msamaha ni mojawapo ya maajabu ya neema ya Mungu. Nguvu yake ya uponyaji ni ya ajabu. Ikiwa mwanamke amehusika katika utoaji mimba, Mungu hahitaji kwamba atembee maisha yake yote akiwa na alama nyekundu “A” kifuani mwake. Anahitaji atubu dhambi zake na aje kwake kwa utakaso wa msamaha. Mungu anapotusamehe, tumesamehewa. Mungu anapotutakasa, tunakuwa safi. Hiyo ni sababu ya kusherehekea sana.
Makala haya yalichapishwa awali kwenye Blogu ya Ligonier Ministries.


