Je, Mungu Hukubali Ibada za Dini Zote?

7 July 2026

Je, Inamaanisha Nini Kuwa “Ndani ya Kristo”?

21 July 2026

Je, Mungu Hukubali Ibada za Dini Zote?

7 July 2026

Je, Inamaanisha Nini Kuwa “Ndani ya Kristo”?

21 July 2026

Yesu Alitoa Ahadi gani Kabla ya Kupaa Kwake?

Ahadi ya mwisho ambayo Yesu aliwapa Mitume wake kabla ya kupaa kwake mbinguni ilikuwa ahadi kwamba Roho Mtakatifu atawajia ili kuwapa nguvu ya kupeleka injili hadi miisho ya dunia (Matendo 1:8). Luka anarekodi utimilifu wa ahadi hii kuanzia Matendo 2, ambayo inatuambia jinsi Roho alivyoshuka juu ya kanisa wakati wa Pentekote.

Chini ya agano la kale, Pentekote ilikuwa moja ya sherehe kuu tatu za hija ambazo zilihitaji Waisraeli kwenda Yerusalemu (Kumbukumbu la Torati 16). Pia iliitwa Sikukuu ya Majuma kwa sababu ilifanyika kwa siku hamsini, au majuma saba, baada ya Sikukuu ya Malimbuko, ambayo iliadhimishwa siku ya kwanza baada ya Sabato ya kwanza wakati wa juma la Pasaka. Pentekote iliashiria mwisho wa mavuno ya nafaka za masika chini ya agano la kale (Walawi 23:4–22). Kwa muda, Wayahudi walihusisha Sikukuu ya Pentekote na utoaji wa sheria katika Mlima Sinai, labda kwa sababu takriban siku hamsini zilikuwa zimepita kati ya kutoka Misri na kupokea sheria (Kutoka 19:1).

Kuingia katika agano jipya, Roho Mtakatifu alikuja juu ya watu wa Mungu siku ya Pentekote iliyofuata mara baada ya kifo na ufufuo wa Yesu. Roho alikuja na sauti ya “upepo wenye nguvu unaovuma.” Neno la “roho” katika Kigiriki na Kiebrania ni neno lilelile linalotafsiriwa kama “upepo,” na Maandiko yanazungumzia kazi yenye nguvu ya Roho Mtakatifu kwa neno upepo au pumzi yenye nguvu (Ezekekieli 37:1–14; Yohana 3:8). Pamoja na sauti ya upepo, ndimi za moto zilizoonekana zikikutua juu ya vichwa vya watu (Matendo 2:3). Moto ulionyesha uwepo wa kiungu na ubatizo wa utakaso ulioahidiwa wa Masihi (Kutoka 3:1–6; Luka 3:15–17).

Bila shaka, Roho Mtakatifu alikuwa pamoja na jumuiya ya agano kabla ya siku ya Pentekote ya agano jipya, kwa maana aliwazaa upya washiriki wa agano la kale na kuwapa kipawa cha imani. Alilazimika kufanya hivyo kwa sababu njia pekee ambayo mtu yeyote humwamini  Mungu wa kweli chini ya agano lolote ni kwa kuzaliwa mara ya pili kwa Roho (tazama Yohana 3:3). Hata hivyo, tajiriba ya agano jipya ya Roho ni kubwa zaidi, kwani sasa Wakristo wote wanamiliki karama za Roho kwa ajili ya huduma.


Makala haya yalichapishwa awali kwenye Blogu ya Ligonier Ministries.


Ligonier Ministries

Ligonier Ministries

We are the teaching fellowship of Dr. R.C. Sproul. We exist to proclaim, teach, and defend God's holiness in all its fullness to as many people as possible. Our mission, passion, and purpose is to help people grow in their knowledge of God and His holiness.