Yesu ni Daudi Mpya

25 August 2026

Yesu ni Daudi Mpya

25 August 2026

Je, Tunaweza Kuiamini Biblia?

Kuna mambo mengi tungeweza kusema ili kuwasaidia Wakristo wenye shaka, au wasio-Wakristo wenye shaka, waiamini Biblia. Tunaweza kuonyesha kwamba Yesu Kristo ametajwa mara kadhaa nje ya Biblia—ikiwemo vyanzo vya Kirumi kama vile Suetonius, Tacitus, na Pliny Mdogo, na vyanzo vya Kiyahudi kama Josephus na Talmud. Tunaweza kutaja ushahidi wa akiolojia wa takribani nusu karne uliothibitisha kuwapo kwa Pontio Pilato, Bwawa la Siloamu, na mji wa Geresa ulioko kandokando ya Bahari ya Galilaya. Tunaweza kuzungumzia ushahidi wa nakala za kale za Biblia, ambao kwa kweli ni bora zaidi kwa mbali kuliko ushahidi wa kitabu kingine chochote cha kale.

Hizi zote ni njia zenye thamani za kufuatilia linapokuja suala la kuchunguza uaminifu wa Biblia. Hata hivyo, nataka kuchukua mkondo tofauti na rahisi zaidi: Nataka kuchunguza Yesu mwenyewe alifikiri nini kuhusu Biblia. Bila shaka, kunukuu Biblia pekee hakutawathibitishia wasioamini kwamba Biblia inategemeka. Mamlaka ya Maandiko, hatimaye, ni suala la ushuhuda wa ndani wa Roho Mtakatifu na kazi ya kimiujiza ya Mungu, ambamo kondoo huisikia sauti ya Mchungaji wao ndani ya Maandiko. Hata hivyo, twaweza kuonyesha kwamba ikiwa, kwa namna yoyote ile, tunamwamini Yesu, basi tunalazimika kuamini pia kwamba Biblia inategemeka. Fikiria vifungu vinne vinavyodhihirisha jinsi Yesu alivyoona  Maandiko.

Mathayo 5:17–19. Hapa katika Hotuba ya Mlimani, Yesu anatangaza kwamba hakuja kubatilisha chembe hata moja wala nukta moja kutoka katika Torati wala Manabii. Kwa kutaja kwake alama hizi ndogo za maandishi kunadhihirisha kuwa anazungumzia Maandiko. Ni rahisi tu kutaka kuweka kando chochote kutoka katika Neno la Mungu kama unavyoweza kuondoa mbingu na nchi.

Mathayo 12:38–42. Katika mabishano yake na waandishi na Mafarisayo, Yesu anamrejea simulizi ya Yona kama historia ya kweli. Yesu haregelei tu kama hadithi ya kubuni. Watu wa Ninawi hawawezi kusimama kuhukumu katika siku ya mwisho iwapo ni wahusika wa kufikirika tu.  Kote katika Injili, Yesu huwachukulia wahusika na historia ya kibiblia—tangu Abeli, Nuhu, na Ibrahimu hadi Eliya, Elisha, na mjane wa Sarepta—kama watu wa kweli waliotokea katika matukio ya kweli ya kihistoria.

Mathayo 19:4–5. Yesu ananukuu Mwanzo 2 kama yale “aliyewaumba … alisema.” Andiko la Mwanzo 2 halijumuishi nukuu ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Lakini hili si tatizo kwa Yesu: Ukweli kwamba ananukuu kutoka katika Biblia unamaanisha kuwa anamnukuu Mungu. Kwa Yesu, kisemacho Biblia ndicho asemacho Mungu.

Yohana 10:35. Hapa Yesu anasema kwa uwazi kabisa kwamba “Maandiko hayawezi kuvunjwa.” Yesu anajadili neno moja tu katika Zaburi 82. Hata hanukuu simulizi la kutoka Misri au mstari maarufu wa Agano la Kale. Anarejelea neno moja katika zaburi isiyotambulika sana. Hata hivyo, Yesu anaamini—naye anaweza kutamka bila kuogopa kupingwa na Myahudi wa kweli—kwamba hakuna neno katika Maandiko linaloweza kuvumjwa. Yesu anafundisha—au bora zaidi, anakadiria kile ambacho kila mtu tayari alikielewa—kwamba hakuna jambo lolote linalofundishwa katika Biblia linaloweza kuwekwa pembezoni, kubatilishwa, au kufutuliwa mbali.

Tufikirieje kuhusu Biblia? Bila shaka, jibu linalofaa kwa Wakristo ni hili: tuamini kuhusu Biblia zetu kile ambacho Yesu aliamini kuhusu Biblia Yake. Yesu alithibitisha kila chembe ya sheria, unabii, simulizi, na mashairi katika Maandiko. Alitetemeka alipofikiria mtu yeyote kupindua, kukataa, au kutokwamini sehemu yoyote ya Maandiko. Kwa furaha alikumbatia mamlaka na ufunuo wa Maandiko hadi kwenye sentensi, kwenye vifungu, kwenye maneno, kwenye herufi ndogo kabisa, hadi kwenye nukta ndogo mno. Yesu alikubali mpangilio wa matukio, miujiza, na historia ya Biblia kama mambo ya kweli moja kwa moja.

Hakuna shaka kwamba Yesu aliamini katika uaminifu kamili wa Maandiko—katika kila jambo na katika kila ukweli unaokusudiwa kuthibitishwa nayo. Na ikiwa Yesu aliamini Biblia, sisi ni nani tudai vinginevyo?

Makala haya yalichapishwa awali kwenye Blogu ya Ligonier Ministries.

Kevin DeYoung

Kevin DeYoung

Rev. Kevin DeYoung is senior pastor of Christ Covenant Church in Matthews, N.C., and associate professor of systematic theology at Reformed Theological Seminary in Charlotte, N.C. He is author of many books, including Just Do Something.

Hamasa kwa ajili ya Upendo

21 July 2026

Je, Kanisa Limejaa Wanafiki?

4 August 2026