Neno Kafanyika Mwili:
Tamko la Ligonier Kuhusu Kristolojia

Tunaungama siri na ajabu
Ya Mungu aliyefanyika mwili
na kufurahia wokovu wetu mkuu
kupitia Yesu Kristo Bwana wetu.

Pamoja na Baba na Roho Mtakatifu,
Mwana aliviumba vitu vyote,
huvihimili vitu vyote,
na huvifanya vitu vyote kuwa vipya.
Mungu kweli,
alifanyika mwanadamu kweli,
asili mbili katika nafsi moja.

Alizaliwa na Bikira Maria
na akaishi miongoni mwetu.
Alisulubiwa, akafa, na kuzikwa.
Alifufuka siku ya tatu,
akapaa hadi mbinguni,
na atakuja tena
katika utukufu na hukumu.

Kwa ajili yetu,
Aliishika Sheria,
akafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi,
akairidhisha ghadhabu ya Mungu.
Alichukua nguo zetu zilizotiwa unajisi,
Akatupatia
Joho lake la haki.

Yeye ni Nabii wetu, Kuhani, na Mfalme,
akilijenga kanisa lake,
akifanya maombezi kwa ajili yetu,
na akitawala juu ya vyote.

Yesu Kristo ni Bwana;
Tunalitukuza Jina lake takatifu milele.

Amina.