Mambo Matatu Unayopaswa Kujua Kuhusu Zekaria
15 January 2026
Mambo Matatu Unayopaswa Kujua Kuhusu Esta
22 January 2026
Mambo Matatu Unayopaswa Kujua Kuhusu Zekaria
15 January 2026
Mambo Matatu Unayopaswa Kujua Kuhusu Esta
22 January 2026

Mambo Matatu Unayopaswa Kujua Kuhusu Ufunuo

Kina tatiza. Kina zua mabishano. Kina sumbua. Kina tisha. Ikiwa kitabu cha Ufunuo kinakuletea mawazo haya akilini mwako, huko peke yako. Hata hivyo, kusudi la Mungu katika Ufunuo ni kufunua, si kuficha—kutia moyo, si kufadhaisha. Ufunuo unaahidi baraka kwa “yeye asomaye kwa sauti maneno ya unabii huu, na … wale waisikiao, na kuyashika yaliyoandikwa humo” (Ufu. 1:3, msisitizo umeongezwa). Fikiria tukio katika kusanyiko la karne ya kwanza ambalo Ufunuo ulitumwa kwao kwanza: kiongozi mmoja anasimama kusoma maandishi kwa sauti, huku watu mwingine wote wanasikiliza. Wanaweza kuelewa ujumbe wa Ufunuo na kupokea baraka inayohahidiwa kwa kusikia tu ikisomwa kwa sauti na kuchukua ukweli wake moyoni. Vivyo hivyo na sisi tunawza. Ili kupokea baraka, unapaswa kujua mambo matatu kuhusu kitabu hiki cha kilele cha Biblia.

1. Ufunuo unafunua ushindi wa Mwanakondoo katika dunia iliyovurugika.

Mstari wa kwanza wa Ufunuo ni kichwa cha kitabu hiki: “Ufunuo wa Yesu Kristo” (Ufu. 1:1). Neno la Kiyunani linalowakilishwa na “ufunuo” (apocalypsis) linapendekeza kwamba “ufunuo” unahitajika ili tuweze kuona kupitia mwonekano wa juu wa tajiriba zetu na historia ya dunia, na kutambua ukweli wa msingi unaoelezea chanzo chao. Ikiwa tutaona tu dalili za juu juu—ukatili wa vita, majanga ya mazingira, kuporomoka kwa uchumi, njaa na ukosefu wa chakula, magonjwa na kifo—hatutawahi kuelewa kwa nini dunia yetu imecharuka. Ni kuchungulia tu nyuma ya pazia katika ulimwengu wa kiroho ambamo Mungu, ambaye ni mtawala juu ya kila kitu, anapambana na “yule joka kuu . . . yule nyoka wa kale, . . . ibilisi na Shetani” (Ufu. 12:9; 20:2), kunafunua mateso na mafumbo yanayotuzunguka.

Kitabu hiki ni “ufunuo wa Yesu Kristo” kwa namna mbili: Yesu ni wakala anayefunua na pia ni mhusika anayefunuliwa. Kwanza, “Mungu alimpa” Yesu Kristo ufunuo huu “kuonyesha watumishi wake mambo ambayo lazima yatokee hivi karibuni” (Ufu. 1:1). Uhamisho huo kutoka kwa Baba kwenda kwa Mwana aliyefanyika mwili unaonyeshwa katika Ufunuo 4 na 5, ambapo Mwanakondoo anapokea kutoka kwa Mfalme aliye kwenye kiti cha enzi gombo na kisha kuvunja mihuri yake, mmoja baada ya mwingine, kuanzisha na kudhibiti matukio yanayojitokeza katika historia. Mwanakondoo pekee ndiye anayestahili kufunua na kutekeleza ajenda ya Mungu kwa kuwa Mwanakondoo ameshinda kwa kuvumilia kifo cha kikatili ili kuwakomboa “watu kwa Mungu kutoka kila kabila na lugha na watu na taifa” (Ufu. 5:5–10).

Pili, Ufunuo humfunua Yesu Kristo. Yeye si tu Mwanakondoo aliyeshinda kupitia mateso ya ukombozi; Yeye pia ni “mfano wa mwana wa Adamu” anayetembea kati ya makanisa Yake duniani (Ufu. 1:10–20), akitathmini afya yao ya kiroho na kubariki wale wanaosimama imara (sura ya 2–3). Yesu ni uzao wa mwanamke aliyeahidiwa mwanzoni mwa historia (Mwa. 3:15), ambaye alipozaliwa alitishiwa na yule nyoka wa kale lakini akatukuzwa kwenye kiti cha enzi cha Mungu (Ufu. 12:1–6). Damu Yake ilimfukuza mshtaki wetu kutoka mbinguni, ikinyamazisha mashtaka dhidi yetu (Ufu. 12:7–17). Yesu ni Kiongozi wa majeshi ya mbinguni yatakayorudi kumharibu joka, wafuasi wake wa kutisha, na wote wanaoamini uongo wao (Ufu. 19:15–21). Yesu, pamoja na Baba na Roho, ndiye kitovu cha ibada ya wahudumu wa mbinguni wa Mungu, wajumbe wake wa kimbinguni, na viumbe vyote kila mahali (Ufu. 5:9–14; 11:15–18; 14:2–5; 15:3–4; 19:1–8; 21:2–4, 22–24; 22:3–5).

Kwa sababu maono ya Ufunuo yanaonyesha uhalisia wa kutisha wa matokeo yenye sumu ya dhambi katika dunia iliyopotoka, mandhari hayo ya machafuko yanavuta hisia zetu, kama ajali katika barabara kuu. Lakini tukijikita kwenye “miti” (mandhari ya uovu wa kibinadamu na ghadhabu ya kimungu inayochochea), tutakosa “msitu” wa Ufunuo: ukuu na rehema ya Yesu Kristo.

2. Ufunuo kinazungumza kwa “misamiatii” ya picha iliyo na mizizi katika Agano la Kale.

Ufunuo unatoa ujumbe wake kwa mtindo unaofaa kusikika ukisomwa kwa sauti: picha za wazi zilizochorwa kwa kudumu kwenye mawazo yetu. Katika Maandiko yote, Mungu (mwasilishaji mkuu) anachora picha: mchungaji, mwamba, ngome, moto, mume, na kadhalika. Kupitia ndoto zilizojaa picha, Bwana anafunua mipango Yake kwa na kupitia Yusufu na Danieli (Mwa. 37, 41; Dan. 2, 7). Kwa manabii kama vile Isaya, Ezekieli, na Zakaria, Bwana anaonyesha nyuma ya pazia, katika mahakama Yake ya mbinguni, akiwawezesha kuona katika ishara za wazi (pamoja na kusikia kwa maneno) ujumbe Wake kwa watu Wake. Katika ishara za Ufunuo, Mungu anafanya kile ambacho amekuwa akifanya daima.

Ili kuelewa umuhimu wa ishara za Ufunuo, tunahitaji kamusi inayotujulisha msamiati wake wa picha. Kamusi hiyo, iliyoandikwa na Mungu kwa karne nyingi, ni Agano la Kale. Watu binafsi na matukio ya historia ya Agano la Kale (uumbaji, nyoka, kutoka, Musa, Eliya, nk), pamoja na maono yaliyoonyeshwa kwa manabii wa Israeli, ni funguo zinazofungua ishara za Ufunuo. Kwa sababu Kristo anazungumza na makanisa ya karne ya kwanza na kanisa la karne ya ishirini na moja, anatumia mtindo wa picha ambao watu Wake wote, katika kila kizazi, wanaweza kuufikia: matukio ya ukombozi ya Agano la Kale na ishara za kinabii.

3. Kusudi la Kristo kwa Ufunuo ni kuimarisha Wakristo ambao imani na uaminifu wao viko chini ya mashambulizi ya Shetani kupitia mateso, kutengwa, udanganyifu, na ulimwengu wa anasa.

Ufunuo kina sifa ya kuchochea mabishano. Ingawa Yesu aliwaoonya watu wasitafute tarehe, kana kwamba tunaweza kuchunguza siri za kiungu ambazo ziko “juu ya uwezo wetu” (Marko 13:32–35; Matendo 1:7), makundi ya Wakristo bado yanapigana vita juu ya jinsi maono ya Yohana yanavyolingana na matukio ya siku zao. Badala ya kutupatia silaha za vita kwa ajili ya mapambano yetu ya eskatolojia, hata hivyo, Yesu alitoa kitabu cha Ufunuo kwa kusudi la haraka na la utekelezaji zaidi: Kristo analiandaa kanisa lake, ambalo liko chini ya mashambulizi ya nguvu za uovu, ili lisimame imara.

Ufunuo Kinatufunulia mbinu za Shetani na kututia nguvu kupinga mashambulizi ya adui. Mateso ya kikatili na kukataliwa na jamii vinawajaribu watu wa Mungu wakane utii wao kwa Kristo. Kanisa linaweza kudanganywa na walimu wa uongo na kushawishiwa katika hali ya kuridhika na kufanya maelewano kupitia utajiri wa kidunia (Ufu. 2–3). Maono ya Yohana “yanawasilisha” silaha hizi za mashambulizi kama mnyama, nabii wa uongo, na kahaba (Ufu. 13, 17).

Makanisa saba ya Asia yalikuwa mfano mdogo wa kanisa katika enzi zote. Nguvu mbaya za Shetani hubadilika, zikivaa mavazi tofauti katika nyakati tofauti. Haijalishi mashambulizi yake yatakuwa ya namna gani, Shetani tayari ameshindwa (Ufu. 12:7–13; 20:1–3). Kwa hiyo, Mwanakondoo mshindi alitupa kitabu cha Ufunuo ili kutujaza ufahamu, ujasiri, na uaminifu kushikilia Neno lake tunapotarajia kwa hamu baraka ya uwepo wake katika mbingu mpya na dunia mpya (Ufu. 1:3; 22:7, 14).

Makala hii ni sehemu ya mkusanyiko wa Kila Kitabu cha Biblia: Mambo 3 ya Kujua.


Makala haya yalichapishwa kwanza katika Blogu ya Huduma za Ligonier.

Dennis E. Johnson
Dennis E. Johnson
Dkt. Dennis E. Johnson ni profesa mstaafu wa theolojia ya vitendo katika Seminari ya Westminster California na mchungaji msaidizi wa Kanisa la Westminster Presbyterian huko Dayton, Tenn. Yeye ni mwandishi wa vitabu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Walking with Jesus through His Word, Triumph of the Lamb, na Let’s Study Acts.