Mambo Matatu Unayopaswa Kujua Kuhusu Yeremia
8 January 2026
Mambo Matatu Unayopaswa Kujua Kuhusu Zekaria
15 January 2026
Mambo Matatu Unayopaswa Kujua Kuhusu Yeremia
8 January 2026
Mambo Matatu Unayopaswa Kujua Kuhusu Zekaria
15 January 2026

Mambo Matatu Unayopaswa Kujua Kuhusu Yakobo

Waraka ulioandikwa na Yakobo unaanzisha mkusanyiko mdogo unaojulikana kama “katoliki” au Nyaraka za Jumla, ambazo zimepewa jina hilo kwa sababu hazijaelekezwa kwa makanisa maalum au watu binafsi bali kwa (takribani) kanisa lote. Katika jambo hili, barua imeandikwa kwa “makabila kumi na mawili yaliyotawanyika” (Yakobo 1:1), mfano wa kuashiria watu wote wa Mungu waliotawanyika duniani kote. Katika makala hii, tutazingatia mambo matatu ya kujua kuhusu waraka huu.

1. Kaka wa kambo wa Yesu pengine aliandika.

Tuanze na uandishi. Wanaume wanne wanaoitwa “Yakobo” ni wanadaiwa kuwa waandishi. Yakobo, ndugu yake Yohana (wana wa Zebedayo, Mathayo 4:21) alikufa mapema sana kuweza kuwa mwandishi (Matendo 12:2). Yakobo mwana wa Alfayo (Mathayo 10:3) na Yakobo baba yake Yuda (Luka 6:16) hawajulikani sana katika kanisa la awali kiasi cha kujitambulisha tu kama “Yakobo” katika waraka huu. Hii inamwacha Yakobo nduguye Yesu (Mathayo 13:55) kama mgombea anayefaa zaidi. Yakobo huyu alianza kama asiyeamini (Yohana 7:5), lakini kupitia tukio la kushangaza la kukutana na Bwana Yesu aliyefufuka (1 Kor. 15:7), alikuwa nguzo ya kanisa la mwanzo na pengine Mtume (Gal. 1:19; 2:9). Kwa nini utambulisho wa mwandishi ni muhimu?

Kwanza, Yakobo alikuwa amebadilishwa na nguvu ya injili, lakini hata hivyo hatumii uhusiano wake wa kidunia na Yesu kwa ajili ya umaarufu. Anajitambulisha tu kama “mtumishi . . . wa Bwana Yesu Kristo” (Yakobo 1:1). Pili, huyu Yakobo anatoa hotuba muhimu katika Baraza la Yerusalemu, akitumia Amosi 9:11–12 kueleza jinsi kifo na ufufuo wa Kristo vinavyo waunganisha watu wa mataifa na Wayahudi chini ya bendera moja ya imani, si alama za kikabila au matendo ya sheria (Matendo 15:13–21). Alipata tajiriba ya injili na kuihubiri injili. Tatu, Yakobo anaingiza mafundisho ya moja kwa moja kutoka kwa kaka yake Yesu katika barua, kama vile maskini wataurithi ufalme (Yakobo 2:5; Mathayo 5:3–5), kuomboleza na kucheka (Yakobo 4:9; Luka 6:25), kuinua wanyenyekevu (Yakobo 4:10; Mathayo 23:12), na “ndiyo”/”hapana” (Yakobo 5:12; Mathayo 5:34–37). Injili ya kaka yake imekuwa injili yake.

2. Yakobo analenga kuongoza maisha ya Kikristo.

Siyo tu kwamba mwandishi ameundwa binafsi na injili, bali pia malengo yake katika waraka huu. Kutoka kina baba wa kanisa hadi kwa wachambuzi wa kisasa, kumekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu muundo na malengo halisi ya waraka huu kwa sababu haufuati aina ya mantiki thabiti tunayoipata katika kitabu kama vile Warumi. Lakini hiyo haimaanishi kuwa hauna mpangilio kabisa. Ni huru zaidi kwa sababu shabaha yake ni mawaidha ya kimaadili yanayowalenga watu ambao tayari ni ndugu na dada Wakristo (Yakobo 1:9, 16, 19; 5:19). Yakobo anahudumu kama baba wa kiroho akionyesha Wakristo jinsi injili inavyopaswa kubadilisha maisha, akiwashauri wasomaji wake kuchagua njia ya utauwa, si dhambi. Zingatia mifano ifuatayo:

  • Utiifu: Weka neno katika vitendo—usiwe msikilizaji tu (Yakobo 1:2–27).
  • Ushirika: Penda wengine bila ubaguzi—usifanye upendeleo (Yakobo 2:1–13).
  • Utiifu: Weka imani yako katika vitendo—usiwe na imani isiyo na matendo (Yakobo 2:14–26).
  • Ushirika: Tumia mdomo wako kubariki wengine—usitumie kuumiza (Yakobo 3:1–18).
  • Utiifu: Weka utakatifu katika vitendo—usiwe kama dunia (Yakobo 4:1–17).
  • Ushirika: Penda maskini—usitafute utajiri usio wa kiungu (Yakobo 5:1–6).
  • Utiifu: Weka subira katika vitendo—usilalamike katika mateso (Yakobo 5:7–20).

Mwandishi anarejelea mada mbili kuu za utiifu na ushirika kutoka pembe tofauti ili kusisitiza mistari ya kichungaji ya matumizi, siyo kauli za mafundisho. Ikiwa injili itakita mizizi, haya ndiyo matunda inapaswa (au haipaswi) kuzaa.

3. Yakobo anakamilisha—siyo kupinga—barua za Paulo.

Kwa kuzingatia malengo hayo, tunaweza kuangalia tena malalamiko ya Luther kwamba kitabu cha Yakobo kinakosa uwazi wa sheria na injili uliopo katika maandiko ya Paulo. Suala hili linakuja kwa ukali katika Yakobo 2:24: “Unaona kwamba mtu anahesabiwa haki kwa matendo na si kwa imani peke yake.” Kwa juu juu, hili linaonekana kama upingaji dhahiri wa madai ya Paulo kwamba “mtu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria” (Rum. 3:28).

Lakini si haraka hivyo. Madai ya Paulo katika Warumi (na katika Wagalatia) inatoka kwa kutoamini ambapo kushika sheria kunashindwa (Rum. 1:18–3:20), hadi kutangazwa kuwa sawa mbele za Mungu kupitia imani (Rum. 3:21–4:23), hadi kufikia kufanywa wana na utakaso unaotokana na kuhesabiwa haki (Rum. 5–8). Kwa maneno mengine, kauli ya Paulo kuhusu kuhesabiwa haki kwa imani badala ya matendo inaangukia katika madai yake kuhusu jinsi mtu anavyookolewa.

Yakobo anajenga madai tofauti. Anazungumza na wale wanaodai kuwa na imani (Yakobo 2:14) lakini hawana aina yoyote ya upendo wa Kikristo wa kuambatana nayo (Yakobo 2:16). “Imani” kama hiyo si imani ya kweli ikiwa haina “matendo” yanayotokana nayo (Yakobo 2:17). Ni tupu au imekufa, na hivyo haina tofauti na idhini tupu ya utambuzi ambayo hata pepo huitumia (Yakobo 2:19).

Yakobo, kwa ufupi, anajibu swali tofauti: Mtu hufanya nini baada ya kuokolewa? Ninawezaje kuonyesha kwamba imani yangu ni ya kweli? Ingawa anatoa jibu lake kwa maneno makali sana—kupitia “matendo”—ufahamu wake wa msingi hauna tofauti na wa Paulo mahali pengine (angalia Wafilipi 2:12). Ni kwamba tu Paulo bado hajajibu upande huo wa swali anaposhughulika na haki.

Tunapoangalia mambo kwa mtazamo huu, tunaona kwamba Yakobo hapingani na maandiko ya Paulo bali anayakamilisha. Sio waraka wa “majani” zaidi ya maandiko yoyote ya Paulo yanayoonyesha injili kama rasilimali nzuri kwa maisha ya Kikristo.

Makala hii ni sehemu ya mkusanyiko wa Kila Kitabu cha Biblia: Mambo Matatu ya Kujua.


Makala haya yalichapishwa kwanza katika Blogu ya Huduma za Ligonier.

Greg Lanier
Greg Lanier
Dr. Gregory R. Lanier is associate professor of New Testament at Reformed Theological Seminary in Orlando, Fla., and associate pastor at River Oaks Church in Lake Mary, Fla. He is author of several books, including Old Made New, The Septuagint: What It Is and Why it Matters, and a forthcoming commentary on the Gospel of Luke.