Imani na maungamo ya Kiprotestanti
8 July 2025
Ushauri wa Luther kwa Maisha ya Kikristo
15 July 2025
Imani na maungamo ya Kiprotestanti
8 July 2025
Ushauri wa Luther kwa Maisha ya Kikristo
15 July 2025

Siku ya Mageuzo ni nini?

Tukio moja katika siku moja lilibadilisha ulimwengu. Ilikuwa  tarehe 31 Oktoba, 1517. Ndugu Martin, mtawa na msomi, alikuwa amepambana kwa miaka mingi na kanisa lake, kanisa la Roma. Alikuwa amesumbuliwa sana na uuzaji wa msamaha usio wa kawaida. Simulizi  ina kila kitu kinachohitajika katika filamu ya Hollywood. Tukutane na waigizaji.

Kwanza, kuna askofu mchanga—mchanga sana kulingana na sheria za kanisa—Albert wa Mainz. Hakuwa tu askofu wa dayosisi mbili, alitamani pia kuwa askofu mkuu wa Mainz. Hili pia lilikuwa kinyume cha sheria za kanisa. Hivyo basi, Albert alimwomba msaada papa huko Roma, Leo X. wa  familia ya De Medici, Leo X  kwa tamaa  aliruhusu matamanio yake kuzidi uwezo wake wa kifedha.. Wakaingia wasanii na wachongaji, Raphael na Michelangelo.

Wakati Albert wa Mainz alipoomba ruhusa maalum ya kipapa, Leo X alikuwa tayari kufanya makubaliano. Albert, akiwa na baraka za kipapa, angeuza msamaha wa dhambi za zamani, za sasa, na za baadaye. Yote haya yalimchukiza mtawa Martin Luther. Je, tunaweza kununua njia yetu kwenda mbinguni? Luther alilazimika kusema.

Lakini kwa nini tarehe 31 Oktoba? Tarehe 1 Novemba ilikuwa na nafasi maalum katika kalenda ya kanisa kama Siku ya Watakatifu Wote. Mnamo tarehe 1 Novemba, 1517, maonyesho makubwa ya masalia mapya yaliyopatikana yangekuwa huko Wittenberg, mji wa nyumbani wa Luther. Mahujaji wangekuja kutoka kila mahali, wakipiga magoti mbele ya masalia, na kupunguza mamia, ikiwa si maelfu, ya miaka katika tohara. Nafsi ya Luther ilizidi kukasirika. Hakuna hata moja kati ya haya lilionekana kuwa sawa.

Martin Luther, msomi, alichukua kalamu ya manyoya mkononi, akachovya wino wake na kuandika Nadharia Tisini na Tano mnamo tarehe 31 Oktoba, 1517. Hizi zilikuwa na lengo la kuchochea mjadala, kuamsha tafakari ya kina miongoni mwa ndugu zake katika kanisa. Nadharia hizi Tisini na Tano zilichochea zaidi ya mjadala. Nadharia hizi Tisini na Tano zilidhihirisha kuwa kanisa lilikuwa mbali mno na marekebisho yaliyokuwa yakihitajika. Ilihitaji mageuzo. Kanisa—na ulimwengu— kamwe usingekuwa kama ulivyo tena.

Moja ya Nadharia Tisini na Tano za Luther inatangaza tu kuwa, “Hazina ya kweli ya Kanisa ni injili ya Yesu Kristo.” Hilo pekee ndilo maana ya Siku ya Mageuzo. Kanisa lilikuwa limepoteza mtazamo wa injili kwa sababu lilikuwa limefunika kurasa za Neno la Mungu kwa tabaka baada ya tabaka ya mapokeo. Mapokeo pekee mara nyingi huleta mifumo ya matendo, ya kujipatia njia ya kurejea kwa Mungu. Ilikuwa kweli kwa Mafarisayo, na ilikuwa kweli kwa Ukristo wa Kikatoliki wa enzi za kati. Je, Kristo Mwenyewe hakusema, “Nira Yangu ni laini na mzigo Wangu ni mwepesi”? Siku ya Mageuzo inasheherekea uzuri wa furaha ya ukombozi  wa injili ya Yesu Kristo.

Siku ya Mageuzo ni nini? Ni siku ambayo nuru ya injili iling’aa kutoka gizani. Ilikuwa siku iliyoanzisha Mageuzo ya Kiprotestanti. Ilikuwa siku ambayo iliwafanya Martin Luther, John Calvin, John Knox, na Wanamageuzi wengine wengi kusaidia kanisa kurudi kwenye Neno la Mungu kama mamlaka kuu pekee kwa imani na maisha na kuliongoza kanisa kurudi kwenye mafundisho ya utukufu ya kuhesabiwa haki kwa neema pekee, kupitia imani pekee, katika Kristo pekee. Iliwasha moto wa jitihada za umishonari, ilisababisha uandishi wa nyimbo na uimbaji wa waumini, na ilisababisha umuhimu wa mahubiri na kuhubiri kwa watu wa Mungu. Ni sherehe ya mabadiliko ya kitheolojia, kikanisa, na kitamaduni.

Kwa hivyo tunasherehekea Siku ya Mageuzo. Siku hii inatukumbusha kuwa na shukrani kwa ajili ya zama zetu na kwa mtawa aliyegeuka Mwanamageuzi. Zaidi ya hayo, siku hii inatukumbusha wajibu wetu, jukumu letu, la kuweka mwanga wa injili katikati ya yote tunayofanya.


Makala haya yalichapishwa kwanza katika Blogu ya Huduma za Ligonier.

Stephen Nichols
Stephen Nichols
Dkt. Stephen J. Nichols ni rais wa Chuo cha Reformation Bible College na afisa mkuu wa masuala ya kitaaluma wa Ligonier Ministries. Yeye ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwa ni pamoja na Beyond the 95 Theses, A Time for Confidence, na R.C. Sproul: Maisha.