Mahali pa Maombi
19 Juni 2025
Mahali pa Maombi
19 Juni 2025

Maana ya Kuondolewa Dhambi na Upatanisho ni Nini?

xr:d:DAFXk0WDSFg:25,j:45162075609,t:23011320

Tunapozungumzia kuhusu tendo liliofanywa kwa ajili ya wengine yaani upatanisho wa Mungu na binadamu kwa maisha na kifo cha Yesu, maneno mawili ya kitaalamu yanajitokeza tena na tena: Kuondolewa dhambi na upatanisho. Maneno haya yanachochea aina zote za mabishano kuhusu ni lipi linapaswa kutumika kutafsiri neno fulani la Kigiriki, na baadhi ya matoleo ya Biblia yanatumia moja ya maneno haya na mengine yatatumia lile lingine. Mara nyingi naulizwa kuelezea tofauti kati ya upatanisho na kuondolewa dhambi. Ugumu ni kwamba ingawa maneno haya yapo katika Biblia, hatuyatumii kama sehemu ya msamiati wetu wa kila siku, kwa hivyo hatuna uhakika kabisa yanachowasilisha katika Maandiko. Hatuna pointi za kumbukumbu kuhusiana na maneno haya.

Kuondolewa dhambi na upatanisho

Hebu tufikirie kuhusu maana ya maneno haya, basi, tukianza na neno kuondolewa dhambi. Kiambishi awali “Ku” maana yake “nje ya” au “kutoka kwa,” hivyo Kuondolewa dhambi kunahusiana na kuondoa kitu au kuchukua kitu. Kwa maneno ya kibiblia, kunahusiana na kuondoa hatia kupitia malipo ya adhabu au kutoa dhabihu ya upatanisho. Kwa upande mwingine, upatanisho unahusiana na lengo la Kuondolewa dhambi. Kiambishi awali “u” kinamaanisha “kwa ajili” , upatanisho huleta mabadiliko katika mtazamo wa Mungu, ili kwamba aondoke kutoka kuwa na uadui nasi hadi kuwa kwa ajili yetu. Kupitia mchakato wa Kupatanishwa, tunarejeshwa katika ushirika na kibali Naye.

Kwa namna fulani, Upatanisho unahusiana na Mungu anavyotulizwa ghadhabu yake. Tunajua jinsi neno upatanisho linavyofanya kazi katika migogoro ya kijeshi na kisiasa. Tunafikiria kuhusu kile kinachoitwa siasa za upatanisho, falsafa ya kwamba ikiwa una mfalme wa dunia mwenye vurugu aliye huru na anayepiga kelele za vita, badala ya kuhatarisha ghadhabu yake ya ghafla unampa Sudetenland kutoka Czechoslovakia au kipande fulani cha ardhi. Unajaribu kutuliza hasira yake kwa kumpa kitu kitakachomridhisha ili asije katika nchi yako na kukuangamiza. Huo ni udhihirisho usio wa kimungu wa upatanisho. Lakini ikiwa una hasira au umekiukwa, na nikakidhi hasira yako, au nikakutuliza, basi ninarudishwa katika upendeleo wako na tatizo linaondolewa.

Neno lile lile la Kigiriki linatafsiriwa kwa maneno yote mawili kuondolewa dhambi na upatanisho mara kwa mara. Lakini kuna tofauti kidogo katika maneno. Kuondolewa dhambi ni kitendo kinachosababisha mabadiliko ya mtazamo wa Mungu kwetu. Ni kile ambacho Kristo alikifanya msalabani, na matokeo ya kazi ya Kristo ya Kuondolewa dhambi ni kupatanishwa—ghadhabu ya Mungu imeondolewa. Tofauti ni sawa na ile kati ya fidia inayolipwa na mtazamo wa yule anayepokea fidia.

Kazi ya Kristo Ilikuwa Kitendo cha kutuliza ghadhabu

Kwa pamoja, kuondolewa dhambi na upatanisho ni vitendo vya kutuliza ghadhabu. Kristo alifanya kazi yake msalabani ili kutuliza ghadhabu ya Mungu. Wazo hili la kutuliza ghadhabu ya Mungu limefanya kidogo kutuliza hasira ya wanatheolojia wa kisasa. Kwa kweli, wanakuwa na hasira sana kuhusu wazo zima la kutuliza ghadhabu ya Mungu. Wanafikiri ni kumtweza Mungu kuhitaji kutuliza ghadhabu yake, kwamba tunapaswa kufanya kitu ili kumtuliza au kumfurahisha. Tunapaswa kuwa waangalifu sana jinsi tunavyoelewa ghadhabu ya Mungu, lakini hebu nikukumbushe kwamba dhana ya kutuliza ghadhabu ya Mungu inahusiana hapa si na hoja ya pembeni au ya kando ya theolojia, bali na kiini cha wokovu.

Wokovu ni nini?

Hebu niulize swali la msingi sana: neno wokovu linamaanisha nini? Kujaribu kuelezea kwa haraka kunaweza kukupa kuumwa na kichwa, kwa sababu neno wokovu limetumika kwa takriban njia sabini tofauti katika Biblia. Ikiwa mtu ameokolewa kutokana na kushindwa vitani, anapata wokovu. Ikiwa mtu atapona ugonjwa unaotishia maisha, mtu huyo anapata wokovu. Ikiwa mimea ya mtu imerejeshwa kutoka kunyauka hadi kunawiri, imeokolewa. Hiyo ni lugha ya kibiblia, na kweli haina tofauti na lugha yetu wenyewe. Tunaokoa pesa. Bondia anaokolewa na kengele, ikimaanisha ameokolewa kutokana na kupoteza pambano kwa kupigwa, na si kwamba amepelekwa katika ufalme wa milele wa Mungu. Kwa kifupi, tukio lolote la ukombozi kutoka kwenye hatari iliyo wazi na iliopo linaweza kusemwa kuwa ni aina ya wokovu.

Wakati tunapozungumzia wokovu kibiblia, tunapaswa kuwa waangalifu kusema kwamba hatimaye tunakombolewa kutoka kwa nini. Mtume Paulo anafanya hivyo kwetu katika 1 Wathesalonike 1:10, ambapo anasema Yesu “anatukomboa kutoka katika ghadhabu ijayo.” Hatimaye, Yesu alikufa kutuokoa kutoka kwenye ghadhabu ya Mungu. Hatuwezi kuyaelewa mafundisho na mahubiri ya Yesu wa Nazareti bila hili, kwa maana aliwaonya watu mara kwa mara kwamba ulimwengu mzima siku moja utahukumiwa na Mungu. Haya ni baadhi ya maonyo Yake kuhusu hukumu: “Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote atakayemkasirikia ndugu yake, atapaswa hukumu” (Mathayo 5:22); “Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilo maana walilonena” (Mathayo 12:36); na “Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona” (Mathayo 12:41) Theolojia ya Yesu ilikuwa theolojia ya mgogoro. Neno la Kigiriki “mgogoro” linamaanisha “hukumu.” Na mgogoro ambao Yesu alihubiri ulikuwa ni mgogoro wa hukumu inayokuja duniani, ambapo Mungu atamimina ghadhabu Yake dhidi ya wasiookolewa, wasiomcha Mungu, na wasiotubu. Tumaini pekee la kuepuka kumiminiwa ghadhabu hiyo ni kufunikwa na upatanisho wa Kristo.

Kwa hiyo, mafanikio makuu ya Kristo msalabani ni kwamba Alituliza ghadhabu ya Mungu, ambayo ingetuunguza kama tusingefunikwa na dhabihu ya Kristo. Kwa hiyo ikiwa mtu anapinga upatanisho au wazo la Kristo kuridhisha ghadhabu ya Mungu, kuwa makini, kwa sababu injili iko hatarini. Hii inahusu kiini cha wokovu—kwamba kama watu ambao wamefunikwa na upatanisho, tumekombolewa kutoka kwenye hatari kubwa ambayo mtu yeyote anakabiliwa nayo. Ni jambo la kutisha kuangukia mikononi mwa Mungu mtakatifu ambaye ana ghadhabu. Lakini hakuna ghadhabu kwa wale ambao dhambi zao zimeshalipiwa. Huu ndio wokovu.


Makala haya yalichapishwa kwanza Katika Blogu ya Huduma za Ligonier.

R.C. Sproul
R.C. Sproul
Dkt. R.C. Sproul alikuwa mwanzilishi wa Ligonier Ministries, mchungaji wa kwanza wa mahubiri na mafundisho katika Saint Andrew’s Chapel huko Sanford, Fla., rais wa kwanza wa Reformation Bible College, na mhariri mtendaji wa gazeti la Tabletalk. Kipindi chake cha redio, Renewing Your Mind, bado kinapeperushwa kila siku katika mamia ya stesheni za redio ulimwenguni na kinaweza kusikilizwa mtandaoni pia. Alikuwa mwandishi wa vitabu zaidi ya mia moja, vikiwemo The Holiness of God, na Everyone’s a Theologian. Alijulikana ulimwenguni kote kwa utetezi wake mahiri wa Kutokukosea kwa Maandiko na uhitaji wa watu wa Mungu kusimama na ukweli wa Neno lake.