Jinsi ya Kusoma Ushairi wa Kiebrania
10 February 2026
Jinsi ya Kusoma Manabii
17 February 2026
Jinsi ya Kusoma Ushairi wa Kiebrania
10 February 2026
Jinsi ya Kusoma Manabii
17 February 2026

Jinsi ya Kusoma Fasihi ya Hekima

“Hofu ya Bwana ndiyo mwanzo wa hekima” (Mith. 9:10; tazama pia Ayubu 28:28; Zab. 111:10; Mith. 1:7). Ingawa kumekuwa na walimu wengi wenye maarifa wasio Wakristo kwa miaka mingi, hekima yote ya kweli hatimaye hutoka “juu”—yaani, kutoka kwa Mungu wa Utatu (Efe. 1:17; Kol. 2:3; Yak. 3:15, 17). Hekima inaweza tu kupata utimilifu wake wa kweli kwa wale wanaomheshimu na kumwabudu Mungu wa kweli pekee.

Hata hivyo, kuna mengi zaidi yanayohitaji kusemwa, kwa sababu si waumini wote Wakristo wanaonyesha hekima katika maisha yao. Kwa kweli, waumini Wakristo mara nyingi hutenda kwa upumbavu na bila kuwajibika, wakijiletea aibu wenyewe na kwa jina la Mungu (kwa mfano, Ezek. 36:20; Rum. 2:24; 1 Kor. 6:5; 1 Kor. 15:34). Maandiko yanasema kwamba hekima itapewa wale wanaoiomba (Yak. 1:5). Hasa, Roho Mtakatifu amehamasisha vitabu mbalimbali vya hekima kama vile Mithali, Ayubu, na Mhubiri hasa kwa kusudi hili. Mkristo anapaswa kusoma vipi Fasihi ya Hekima kwa faida?

1. Tambua jinsi ilivyo rahisi kuwa na hekima machoni petu wenyewe.

Kwanza, mtu anapaswa kusoma Fasihi ya Hekima kwa kutambua jinsi ilivyo rahisi kwa wenye dhambi kuwa “wenye hekima machoni pao wenyewe.” Kitabu cha Mithali mara nyingi huzungumzia tatizo hili kubwa (Mith. 3:7; 12:15; 26:5; 28:11; pia Isa. 5:21). Hakika, mtu “mwenye hekima machoni pake mwenyewe” yuko katika hali mbaya zaidi kuliko “mpumbavu” wa kibiblia (Mith. 26:12). Ishara za ugonjwa huu wa kiroho ni pamoja na kukataa kusikiliza ushauri wa washauri wacha Mungu (Mith. 26:16)—hasa wazazi wa mtu (Mith. 1:8; 4:1; 23:22; 30:17)—na kusisitiza kushinda kila mabishano (Mhub. 7:15–16). Mtu anapaswa kuwa makini na tabia ya haraka ya “kuimarisha” mtazamo wake anapopingwa na waumini waliokomaa kiroho. Badala yake, Wakristo wanapaswa daima kuonyesha roho ya kujifunza.

2. Tafuta mifumo ya jumla.

Pili, mtu anapaswa kusoma Fasihi ya Hekima ili kujifunza mifumo ya jumla ya jinsi dunia inavyofanya kazi kwa kawaida, na wanapaswa kutenda ipasavyo. Kwa ujumla, wale wanaotembea katika “hofu ya Bwana” na wanaotafuta kutekeleza maagizo ya Mungu hupata viwango vya kustawi “kama mti uliopandwa kando ya mifereji ya maji” (Zab. 1:3). Neno hekima ya kawaida wakati mwingine huchukuliwa kama neno la lawama, lakini kwa kweli, Biblia yenyewe inakusanya hazina ya utajiri wa hekima kama hiyo ili kuipitisha kwa vizazi vinavyofuata vya watu wa Mungu. Wasomaji wanafanya vyema kuzingatia hekima hiyo ya kawaida badala ya kuipuuza na kudhani kwamba watakinzana na sheria za jumla za jinsi mambo yanavyofanya kazi. Mkristo ambaye anafikiri, kwa mfano, kwamba anaweza kustawi kiroho huku akiepuka mikusanyiko ya pamoja ya kanisa anapuuza si tu msukumo wa Maandiko bali pia hekima ya waumini wengi wa miaka mingi ambao wamepata baraka zisizopimika zinazoweza kupatikana tu wakati kanisa linakusanyika kwa jina la Kristo (Math. 18:20).

3. Chunguza upekee wa “sheria.”

Tatu, mtu anapaswa kusoma Fasihi ya Hekima ili kuchunguza “upekee wa sheria,” ambao unaonyesha haja ya utambuzi na utegemezi wa mara kwa mara kwa Bwana. Tajirib ya Ayubu, na mafundisho ya mara kwa mara ya kitabu cha Mhubiri, yanashuhudia kwamba kuna nyakati ambapo mifumo ya jumla ya maisha haitumiki. Hivyo, wakati mwingine, wenye haki wanateseka badala ya kustawi, na wapumbavu wanafurahia ufanisi badala ya kupata shida. Kutaja mfano wa Agano Jipya, kulingana na hali fulani mbaya Biblia inapendekeza waumini wajiepushe na ndoa (1 Kor. 7:25–26), ingawa kwa ujumla inatarajia kwamba waumini wengi watapata “msaidizi anayefaa” ambaye wataanzisha familia na kutawala dunia (Mwa. 1:26–30; Mwa. 2:18–25). Kwa kutambua kwamba kuna upekee katika mifumo ya jumla, muumini anapaswa kukabiliana na kila hali kwa masharti yake yenyewe, kwa maombi, akiomba hekima na utambuzi wa Bwana ili kujua jinsi bora ya kutenda kwa utukufu Wake.

4. Jifunze jinsi ya kutumia utambuzi na kumtengemea Bwana.

Nne, mtu anapaswa kusoma Fasihi ya Hekima ili kujifunza jinsi ya kutambua ni chaguo gani ni “bora” au “bora zaidi” katika hali fulani, sio lazima ni njia gani pekee ni “sahihi” au “mbaya”. Maandiko kwa kweli yanatoa sheria nyingi zisizobadilika kuhusu nini ni sahihi au ni mbaya, au nini kinaamriwa au kupigwa marufuku. Hata hivyo, maamuzi mengi maishani yanahusisha zaidi ya kuzingatia tu nini ni sahihi au si sawa. Kwa mfano, muumini anayekubali hitaji la kibiblia la kuoa “katika Bwana” (1 Kor. 7:39; linganisha 2 Kor. 6:14) bado ana machaguo mengi ya mwenzi. Mkristo atahitaji hekima na utambuzi ili kufikia ni wenza gani wanaoweza kuafaa zaidi kwake. Maamuzi mengine mengi maishani (elimu, kazi, mahali pa kuishi, nk) hayaji kwa chaguo la moja kwa moja kati ya chaguo sahihi au lisilo sahihi, bali kati ya aina mbalimbali za machaguo “zuri, bora, au bora zaidi”. Kwa bahati nzuri, katika Maandiko, Bwana amewapa waumini utajiri mkubwa wa mafundisho ya hekima, na ameahidi baraka ya Roho kwa wale wanaoomba kwa unyenyekevu (Luka 11:13).


Makala hii ni sehemu ya mkusanyiko wa Hemenitiki (taaluma ya ufasiri wa Biblia).

Max Rogland
Max Rogland
Dkt. Max F. Rogland ni mitumishi mkuu wa Kanisa la Rose Hill Presbyterian na profesa msaidizi wa Agano la Kale katika Erskine Theological Seminary huko Columbia, S.C.