Kwa Nini Unafanya Kazi?
23 Juni 2025
Kwa nini Mageuzo Yalikuwa ya Lazima?
1 Julai 2025
Kwa Nini Unafanya Kazi?
23 Juni 2025
Kwa nini Mageuzo Yalikuwa ya Lazima?
1 Julai 2025

Martin Luther Alikufaje?

xr:d:DAFOOw3yt3M:10,j:37241480381,t:22100603

Martin Luther alikufa Februari, tarehe 18 mwaka wa 1546. Mwezi mmoja kabla, aliandika kwa rafiki akilalamika kuhusu udhaifu wa umri wake, “Mimi, mzee, mchovu, mvivu, nimechoka, ninasikia baridi, natetemeka, na, zaidi ya yote, mtu mwenye jicho moja.” Kisha akishusha pumzi, “Nikiwa nusu mfu kama nilivyo, naweza kuachwa kwa amani.”

Hata hivyo, Luther hakuachwa apumzike kwa amani. Mji wake wa nyumbani wa Eisleben ulikabiliwa na mgogoro. Mgogoro ulitishia utaratibu wa kiraia na hata utaratibu wa kikanisa. Akiwa amechoka hivyo, Luther aliamua kusafiri kwenda katika mji wake wa nyumbani ili kutatua mzozo huo. Aliondoka Wittenberg na wanawe watatu, na watumishi wachache. Wakafika Halle. Barafu na dhoruba kulifanya kuvuka mito kuwa changamoto. Luther alitumia muda kuyapa majina mapande ya barafu yaliyokuwa yakielea kuelekea kwa mashua yao, mara akiyaita  ni wapinzani wa Wa-Anabaptisti, na maaskofu na mapapa wa Kanisa Katoliki la Rumi.  Huenda alikuwa nusu mfu, lakini ucheshi wake ulikuwa mzima kabisa.

Halle yalikuwa makazi ya mshiriki wa Luther wa muda mrefu, Dkt. Justus Jonas. Tangu mjadala wa Leipzig mwaka 1519, Jonas alikuwa mmoja wa wanafunzi wa karibu zaidi wa Luther. Jonas alisimama pamoja naye katika Baraza la Worms. Aliendeleza Mageuzo huko Wittenberg, wakati Luther alipokuwa uhamishoni Wartburg. Na sasa Justus Jonas angeandamana na Luther kwenye safari yake ya mwisho.

Luther na kundi lake kubwa la wasafiri waliingia kwa ushindi huko Eisleben. Shujaa wa mji wa nyumbani alipokelewa kwa shangwe za umati wa watu na akasindikizwa na msafara. Alihubiri Jumapili hiyo, tarehe 31, Januari.

Lakini safari ilikuwa imeacha athari zake. Luther alimwandika  mpenzi wake Katie kuhusu upepo mkali na mvua za baridi, bila kusahau mapande yote yale ya barafu yaliyotisha. Luther alikuwa mgonjwa sana. Moto mkali, nje ya chumba cha Luther, pia ulitishia maisha yake. Chumba chake chenyewe kilikuwa na hatari. Plasta ilianguka kutoka kwenye kuta, ambayo ililegeza baadhi ya mawe kutoka kwenye ukuta. Jiwe moja, lililoripotiwa kuwa na ukubwa wa mto, lilikaribia sana kuanguka juu ya kichwa cha 

Luther. Matukio haya ya kutatanisha yalimfanya Katie kuwa na wasiwasi akiwa nyumbani. Alituma barua iliyojaa wasiwasi na hofu. Kwa hivyo Luther aliandika akijibu kwamba alimkosa, akiongeza, “Nina mlezi ambaye ni bora kuliko wewe na malaika wote; amelala kwenye hori na kunyonya kwenye kifua cha mama yake, na bado anaketi mkono wa kuume wa Mungu, Baba Mwenyezi.”

Luther aliandika barua hiyo tarehe 7 Februari. Siku kumi na moja baadaye alikufa. Eisleben, mji wa kuzaliwa kwake, pia sasa ungetambulika kama mji wa kifo chake. Wana watatu wa Luther wangesafiri na mwili wa baba yao kurudi Wittenberg, ambako umati ungekusanyika kutoa heshima za mwisho.

Kabla tu ya kufariki, Luther alihubiri yale yangekuwa mahubiri yake ya mwisho akiwa katika kitanda chake cha mauti, mjini Eisleben. “Mahubiri” yalihusisha kunukuu maandiko mawili, moja kutoka Zaburi na moja kutoka Injili. Luther alinukuu Zaburi 68:19, “Na ahimidiwe Bwana, anayetuchukua kila siku; Mungu ni wokovu wetu.” Kisha alinukuu Yohana 3:16. Mungu wetu kwa kweli ni Mungu wa wokovu, na wokovu huo huja kupitia kazi ya Mwana wake.

Lucas Cranach, mchoraji, alitoa kumbukumbu ya mwisho kwa rafiki yake. Mchoro huo unapamba madhabahu katika Kanisa la Castle. Katika huo mchoro, Luther anahubiri huku umati ukisikiliza. Cranach alimchora mke wa Luther, Katie, kwenye picha hiyo pia. Pia alimchora binti wa Luther, Magdalena, ambaye alikufa alipokuwa na miaka kumi na mitatu, kwenye picha hiyo. Kati ya Luther na kusanyiko lake yupo Kristo. Luther alihubiri Kristo, na Kristo aliyesulubiwa. Na wakati waumini wake walipomsikia Luther akihubiri, hawakumwona Luther bali walimwona Kristo na Kristo Aliyesulubiwa. Huo ndio urithi wa Luther.

Na urithi huo unaenea mbali zaidi ya siku za maisha ya Luther mwenyewe.

Mnamo mwaka wa 1940, W. H. Auden alitoa heshima ya kishairi kwa Luther na urithi wake. Alilipa shairi lake fupi jina “Luther,” akimalizia na mistari hii:

Kazi Zote, Watu Wakuu, Jamii ni mbovu.

“Wenye haki wataishi kwa imani…” alilia kwa hofu.

Na wanaume na wanawake wa ulimwengu walifurahi,

Ambao hawajawahi kujali au kutetemeka maishani mwao.


Makala haya yalichapishwa kwanza katika Blogu ya Huduma za Ligonier.

Stephen Nichols
Stephen Nichols
Dkt. Stephen J. Nichols ni rais wa Chuo cha Reformation Bible College na afisa mkuu wa masuala ya kitaaluma wa Ligonier Ministries. Yeye ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwa ni pamoja na Beyond the 95 Theses, A Time for Confidence, na R.C. Sproul: Maisha.