Dhamira zisizoyumba
Ijapo dunia inayotuzunguka inabadilika kila wakati, tunajitahidi kuendelea na safari, kuendeleza mwamko wa kimataifa wa kihistoria wa imani ya Kikristo. Ligonier Ministries imerasimisha dhamira hizi kumi kuelekea mwisho huo, tukitegemea neema ya Mungu ili tusiyumbeyumbe tunapoongoza misheni hii tuliyokabidhiwa.
1. Kuendelea kuwa na msimamo na dhamira jasiri kwa Ukristo wa Kihistoria.
Hatutabadilika katika nyakati zinazobadilika. Badala yake tutapata nguvu kutoka kwa mamlaka ya Biblia na utoshelezi wa msalaba wa Kristo. Tunachota kutoka kwenye utajiri wa mafundisho ya imani ya kihistoria ya Kikristo kusaidia watu wengi iwezekanavyo kunawiri katika familia zao, makanisa, kazi, jumuiya na mataifa yao.
Lengo letu ni kwa Wakristo waishi kwa kusadikika, na kuweza kustahimili changamoto za kidunia, dini za uongo, na uateisti wa mapambano. Tunajali mateso yote, hasa mateso ya milele, na msukumo wa agizo kuu la kufanya wanafunzi unahuisha uhamasishaji wetu wote.
2. Zingatia Theolojia, Theolojia, Theolojia
Jambo la kupendeza sana tunaloweza kuwapa watu ni ukweli. Dkt. R. C. Sproul alisema kuwa mawazo mema hutangulia kuishi kwema. Tunavyofikiri kumhusu Mungu hutuumba tulivyo, kupenya hadi katika msingi wa imani zetu na kuamua maadili, malengo na maamuzi yetu. Theolojia ni kumjua Mungu ni nani ili tuweze kumwabudu na kumfurahia. Kwa neema ya Mungu, tutaendeleza dhamira isiyoyumba kwa ukweli ambao unatuwezesha kuishi kwa uaminifu na kutoa matunda kwa manufaa ya kila kabila, lugha, na taifa.
3. Ekeza Katika mfumo wa Sauti na Video
Siku zote tumekua waanzilishi katika video za elimu ya Kikristo. Leo tunakuza uwezo wa studio zetu, tukikaribisha wataalamu wajuzi zaidi, na kuongeza kina cha maktaba yetu ya elimu ya Kikristo iendelee kutoa mafundisho yanayoaminika katika soko ambalo limejaa makosa. Wakati huo huo, tunawekeza vikubwa katika podikasti mpya na matangazo ya redio ili kufaidika kutokana na mfufumko wa hivi karibuni wa kusambaza maudhui kupitia vifaa vya sauti.
4. Kuchapisha kwa ajili ya kila hatua ya maisha ya Kikristo
Usomaji wa Biblia ulimwenguni kote ni duni sana. Fasihi yetu inayoeleza aina za uanafunzi hueneza ukweli wa Neno la Mungu kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Mafundisho yetu ya Biblia, gazeti la mafundisho ya Biblia ya kila mwezi, vitabu kutoka kwa waandishi wanaoaminika, kumbukumbu za makala mtandaoni, na zaidi zinaendelea kuwa nyenzo za kwanza ambazo watu huchukua wanapofahamu uhalisia wa kuwa Mungu ni nani na jinsi anavyotaka waishi.
5. Kukusanya Wakristo katika Jumuiya
Chuma hunoa chuma, kwa hivyo Wakristo lazima watiane moyo wampende Mungu kwa mioyo, roho, akili na nguvu zao zote. Tunawakusanya waumini kwa makongamano, matukio ya mafundisho yenye ukaribu mno, na programu kali za elimu katika chuo chetu cha Biblia cha Orlando, kwa sababu hakuna mtu aliyenuiwa kukua katika hali ya kujitenga. Tunampenda na kumtumikia Mungu vyema tunapokua Katika jumuiya.
6. Kutumia Teknoljia inayoibuka
Paulo alitumia barabara za Rumi kusambaza barua zake, Martin Luther alitumia mapinduzi ya uchapishaji ya Gutenberg, na Dkt. Sproul alitambua kwamba kupitia matumizi ya hekima ya teknolojia mpya, masafa yanaweza kupunguzwa na vizuizi vya lugha kuvunjwa. Kukiwa na rununu katika kila mfuko, tutaendeleza msisitizo wa matumizi bunifu ya mtandao ili kuongeza ufikiaji wa huduma zetu.
7. Kukabiliana na kushughulikia mahitaji ya Kieneo
Kwa sababu kuna njaa ya ukweli wa Mungu ulimwenguni, Ligonier si huduma ya Kiingereza pekee. Tunakutana na kujifunza mahitaji maalumu ya Wakristo ulimwenguni na halafu kueneza mafundisho ya uanafunzi katika lugha na nchi tofauti tofauti ili kuzisaidia familia, makanisa, na shule kukua Katika Kristo.
8. Kutafuta washirika wa Kimataifa wanaoaminika
Hakuna huduma inayoweza kufanya kazi inayofanya peke yake. Tunatafuta viongozi wa makanisa, wamishenari, na mashirika yaliyo na mawazo sawa na yetu katika sehemu kadhaa ambao hutumikia vikundi mbalimbali vya watu. Tunajijua sisi ni nani, na shukurani kwa wafadhili wetu wenye maono, kwa njia ya kipekee tunaweza kupeleka nyenzo za uanafunzi za kuaminika kwa watu popote walipo.
9. Kuwaandaa Wachungaji na Viongozi
Tunasaidia kunoa makali ya wahubiri wa Neno la Mungu. Wanahitaji fursa ya mikakati ya kutiwa nguvu, nasi hufanya hivi kupitia semina na makongamano ya mahubiri pamoja na fursa za kipekee za kukua kwa Wakristo.
10. Kufikia kizazi kijacho
Dkt. Sproul alikita mtazamo wetu kama huduma alipotutaka kila mmoja wetu “kufikia watu wengi iwezekanavyo” na ujumbe wa utakatifu wa Mungu na ukweli wa Neno lake. Kufikia kizazi kijacho ni muhimu. Tunajishughulisha na vyuo na wanafunzi wa shule za upili, tukiwafundisha wajue wanachokiamini, kwa nini wanakiamini, jinsi ya kuishi ndani yake, na namna ya kukisambaza. Tunafanya hivi katika makanisa, mashule na vyuo vikuu, katika vyuo vyetu na kupitia app na mtandao. Mazungumzo Makuu ya mawazo yamekuwa Makabiliano Makuu kati ya ukweli na makosa, aidha hatima ya milele ikiwa hatarini. Siku za usoni ni za Wakristo wenye imani. Tuna nia ya kuwepo kusaidia katika vita kwa roho za Vijana wetu.
Kutangaza, kufundisha, na kutetea utakatifu wa Mungu katika ukamilifu wake ndiyo pigo la moyo la Ligonier. Asanteni kwa kuzingatia kwa maombi jinsi Bwana atakavyowawezesha kusaidia huduma hii tunapotafuta mwamko wa kimataifa kumhusu Mungu wetu Mtakatifu na Neno Lake takatifu.