Kupata Tumaini Katikati ya Ugonjwa Mbaya

2 June 2026

Jinsi ya Kukabiliana na Uchovu katika Huduma

9 June 2026

Kupata Tumaini Katikati ya Ugonjwa Mbaya

2 June 2026

Jinsi ya Kukabiliana na Uchovu katika Huduma

9 June 2026

Jinsi Gani Ninaweza Kukabiliana na Kukata Tamaa?

Ikiwa tumaini ni kutamani maisha, kukata tamaa ni kutamani mwisho. Kama Eliya chini ya mti wa mretemu(1 Wafalme 19:1–10), Ayubu akijutia kuzaliwa kwake (Ayubu 3), au Paulo, aliyekuwa amelemewa sana na mateso kiasi cha kukata tamaa ya kuishi(2 Wakorintho 1:8), waumini waliozaliwa katika tumaini hai wanaweza kujihisi wamenaswa katika nyakati za maumivu makali. 

Mwandishi wa zaburi alilia,

Maporomoko yako yote na mawimbi yako

yamepita juu yangu. (Zaburi 42:7)

Ayubu alilalamika, “Roho yangu imevunjika; siku zangu zimekoma” (Ayubu 17:1). Hizi siyo tu kauli za kishairi—zinadhihirisha hali halisi ambapo mateso yanaweza kuvuka kile tunachoweza kustahimili.

Kukata tamaa hakuji tu kwa wale tunaoweza kufikiria wanaweza kufikiwa: wale wenye huzuni, wasioridhika, au wale wenye ufahamu mdogo. Hapana, hata watakatifu wenye nguvu kama Charles Spurgeon, Martyn Lloyd-Jones, na John Bunyan walipitia misimu ya maumivu makali na uchungu. Hakubagui kulingana na tabia au ukomavu wa kiroho.

Mtu aliye katika hali ya kukata tamaa anataka jambo moja tu: kupata nafuu kutoka katika hali hiyo. Asili hasa ya mapambano ni udanganyifu wenye nguvu wa kushindwa na kutokuwa na maana bila suluhisho au njia ya kutoka. Mwandishi wa zaburi alielezea hivi:

Nimeingia katika maji ya kina,

na mafuriko yamenigharikisha. (Zaburi 69:2)

Kama kuogelea katika bahari yenye dhoruba, inaweza kuhisi kama tunazama mbele ya macho, karibu ya kufikiwa na waokoaji.

Iwapo ni kushuka taratibu au kusukumwa ghafla kwa akili na roho hadi ukingoni, kukata tamaa kunapotosha uhalisia wa tumaini la muumini na kupunguza uwezo wa mwili, akili, na roho. Urejesho, basi, unahusisha mtazamo na uwezo uliorejeshwa tunapomtegemea Kristo katika udhaifu wetu na kutumia imani kupitia hatua “ndogo” za utiifu, uvumilivu, na tumaini ambayo inavunja kasi ya kukata tamaa.

Kukatiza Tafakari

Katika kitabu cha Bunyan, The Pilgrim’s Progress, wakati Christian alipokuwa akidhoofika katika kasri la Giant Despair, giza halikuwa udanganyifu; lilikuwa uhalisia wa kushikika na wa kukandamiza. Vivyo hivyo, tunaweza kuwa katikati ya hali mbaya sana, lakini kukata tamaa kunatufanya tuzizunguke bila kikomo huku tukiziba tumaini letu katika Kristo. Ukombozi wa Christian haukuja kwa sababu giza lilimalizika bali kwa sababu alikumbuka kutumia ufunguo wa ahadi mfukoni mwake.

Neno la Mungu linahitaji kukatiza na kubadilisha mawazo yetu mara kwa mara. Wakati kuachwa kunapokaribia, kumbuka kwamba Ameahidi kutokuacha kamwe au kukutupa. Wakati vilindi vinaonekana kuwa Mungu hawezi kuvifikia, kumbuka kwamba Alishuka hadi Sheol yenyewe. Wakati hujui la kuomba, jua kwamba Roho anaugua kwa niaba yako. 

Kujali Mwili

Wakati Eliya alihisi kulemewa, Mungu alimpa chakula, pumziko, na uwepo Wake. Tumeumbwa tukiwa na uwezo wenye mipaka ambao huhitaji kurejeshwa nguvu unapochoka au kuisha. Kwa hiyo, unyenyekevu unahitaji mazoezi ya kila siku, kupata usingizi wa kutosha, kuilisha miili yetu vizuri, kupata mwanga wa jua, kutafuta huduma za matibabu, na kujipumzisha badala ya kujilazimisha kuendelea na majukumu. Ingawa kushughulikia mahitaji yetu ya kimwili kunaweza kuonekana kuwa jambo dogo au lisilo na maana, kwa kweli ni tendo lenye nguvu la utiifu, kuheshimu mipaka ya uumbaji wetu na kuutumaini utoaji wa Mungu. 

Kuwageukia Wengine

Kama vile silika ya kuishi ilivyo, kukata tamaa kuna tawala kila sehemu ya anayeteseka, ikidai kujitazama binafsi na kujitenga na wengine. Mwelekeo wenye nguvu wa kujichunguza kwa namna iliyopotoka unaweza kupunguzwa kwa kutoa na kupokea muda, kujali, na kuwepo pamoja na wengine.   Ni vizuri kuwaacha wengine waingie, sio tu kupokea upendo bali pia kuutoa kupitia mazungumzo na kujishughulisha. Matendo madogo ya kujali huwatanguliza wengine na hufanya kazi kama kinga thabiti dhidi ya mvuto wa kibinafsi. Waombee walio karibu nawe, tuma ujumbe wa kuwatia moyo, elekeza mazungumzo yakuwahusu wao—yote haya ni njia zinazokuweka huru na kurejesha mtazamo wa kumwelekea Mungu na jirani.

Uokoaji kupitia Utaratibu wa shughuli za kila siku

Wakati kukata tamaa kunatuondolea kila kitu isipokuwa mahitaji ya msingi ya maisha, tuyakumbatie haya mahitaji ya msingi kama sehemu ya uokoaji wetu. Shughuli za kila siku, haijalishi ni ndogo kiasi gani, huleta mpangilio. Kazi rahisi kama kuamka kila asubuhi, kufua nguo, au kukata nyasi zinakuwa njia za kawaida na kusudi. Hata kama jitihada zinaonekana za kujirudiarudia, kukumbatia jambo linalofuata ni kitendo cha matumaini. Uaminifu katika mambo madogo (Luka 16:10) hujenga upya uwezo wetu na kuthibitisha maana na kusudi, kubadilisha mambo ya kawaida kuwa uokoaji.

Faraja ya Uumbaji

Wakati hofu kubwa inapotawala, kukumbuka udogo wetu mbele ya ukuu na enzi kuu ya Mungu kunaleta nafuu. Yeye hushikilia uumbaji wote pamoja, ikiwemo nasi. Kukata tamaa kwa Ayubu kulikageuka kuwa ibada wakati Mungu alipoonyesha tabia Yake na enzi yake Kuu kwa kushikilia kila kitu kuanzia ukanda wa Orion angani hadi milango ya bahari. Unapozuru mazingira, kulala chini ya nyota, kupanda maua, kutunza wanyama—uzuri wa uumbaji hutufariji na kurekebisha mtazamo wetu huku Akituhudumia kupitia dunia ya asili. 

Stahimili kwa Uvumilivu

Wakati giza linapoendelea na nafuu haiji, kumbuka kwamba mchakato kutoka katika mateso hadi matumaini unahitaji uvumilivu. Hii inamaanisha muda na imani. Kuishi katika mvutano si rahisi, lakini udhaifu na uhitaji ni masharti ya kujifunza kumtegemea Kristo kikamilifu. Ametuita si tu kushiriki katika ushindi na nguvu za ufufuo wake, bali pia katika ushirika wa mateso yake (Wafilipi 3:10). Endelea kustahimili katika hatua hizo za imani zinazopungua nguvu—hizo ndizo kazi njema alizokuandalia ufanye katika kipindi hiki.  

Usiogope vivuli. Ingawa vinaonekana kutokuwa na mwisho, ukweli ni kwamba ni “kwa muda kidogo [mpaka] Mungu wa neema yote, aliyekuita kwenye utukufu wake wa milele katika Kristo, atakurejesha, atakuthibitisha, atakutia nguvu, na kukuweka imara” (1 Petro 5:10). Vivuli vinaweza kuendelea kuwa na kina, lakini havitaweza kamwe kudai wale ambao wameokolewa kutoka kwenye utawala wa giza na kuhamishwa katika ufalme wa Mwana (Wakolosai 1:13).


Makala haya yalichapishwa awali kwenye Blogu ya Ligonier Ministries.

Kara Dedert

Kara Dedert

Marissa Henley ni mzungumzaji wa matukio na mwandishi wa Loving Your Friend Through Cancer and After Cancer. Anaandika kwenye MarissaHenley.com.