Nawezaje Kukua Katika Imani Yangu?
14 April 2026
Nawezaje Kukua Katika Imani Yangu?
14 April 2026

Ufuasi katika Familia

Hakuna maandiko ya Biblia yanayozungumzia ufuasi yanayostahili kupewa umakini zaidi kuliko Agizo Kuu. Agizo hilo, au amri, linatolewa kwa wanafunzi (Math. 28:16) ili kuwafanya wanafunzi (Math. 28:19–20). Na Yesu anatoa jinsi ya kufanya hivyo: ubatizo wa Kikristo na mafundisho ya kibiblia. Kabla ya mzazi kufanya chochote kumwadhibu mtoto, ni vyema azingatie mpango wa Kristo wa kufanya wanafunzi. Nidhamu ya Kristo lazima iwe tabia ya nyumba zetu. Hiyo hakika inahusisha kuwarudi watoto kwa namna tunavyofikiria mara nyingi (Mith. 13:24; 19:18; 22:15; 23:13–14; 29:15–17), lakini pia inahitaji mengi zaidi kutoka kwa wazazi.

Bila kusoma Mithali kwa makini katika muktadha wa Maandiko yote, tunaweza (na mara nyingi tunafanya) kuangukia katika nadharia ya tabia, mbinu ya kisaikolojia ya kidunia inayochukulia kujifunza kwa binadamu ni kama suala la kuzoea matokeo tu. Lakini Kristo anatufundisha kwamba sisi na watoto wetu ni zaidi ya hayo. Tuna mioyo, vituo vya kiroho vya uwepo wetu, ambako tabia zetu hutoka (Mith. 4:23; Math. 12:33–35; 15:10–20; Luka 6:43–45). Biblia pia inafundisha kwamba mioyo yetu inazaliwa katika uovu (Zab. 51:5; Rum. 5:12), hivyo basi washiriki wa familia—wazazi na watoto—hatimaye wanahitaji kutatuliwa matatizo yao kutoka ndani kwenda nje.

Hili linawarudisha wazazi kwenye Agizo Kuu. Hitaji la msingi la ufuasi ni moyo mpya uliosafishwa kutoka dhambini. Ni Kristo pekee anayeweza kutimiza kazi hii. Bwana, akizungumza kupitia nabii Ezekieli, anasema, “Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtatakata uchafu wenu wote na sanamu za miungu yenu yote. Nitawapeni moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu. Nitauondoa kwenu moyo mgumu kama jiwe na kuwapa moyo wa utii. Nitatia roho yangu ndani yenu; nitawafanya mfuate kanuni zangu na kuzingatia maazimio yangu..” (Ezek. 36:25–27). Uhusiano na ubatizo katika Agizo Kuu ni dhahiri. Iwe mtu anakubali ubatizo wa waumini au ubatizo wa watoto wachanga, kila mtu anakubaliana kwamba ubatizo ni kitu kinachofanywa kwa ajili yako, si kitu unachojifanyia mwenyewe. Ni ishara ya nje inayoashiria umuhimu wa kazi ya Roho. Wazazi Wakristo lazima wajue hili: hakuna ufuasi wa kweli unaokuja bila mabadiliko ya moyo. Mwanzo wa ufuasi kwa watoto wetu hauwezi kutenganishwa na ubatizo.

Kwa matarajio ya Bwana kufanya mabadiliko ya moyo ndani ya watoto wao, kisha wazazi wanaweza kuendelea na kazi ya “kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru” (Math. 28:20). Tena, huku si tu ulinganifu wa tabia kwa watoto wadogo. Wazazi wanawaadhibu watoto wao kwa haki kwa sababu ianayofaa kwa kutoheshimu, vurugu zisizo za haki, uasherati, wizi, uongo, na kutoridhika; na hiyo pia itajumuisha neno la kukemea (Mith. 29:15). Lakini sheria pia  kwanza inamlenga Mungu (amri nne za kwanza, Kut. 20:2–11).

Wazazi wanapaswa kukumbatia “yote niliyowaamuru.” Hii inajumuisha mwito wa Kristo wa uaminifu usioyumba (Yohana 14:6; Luka 10:27) pamoja na kujikana na upendo kwa wengine (Mathayo 16:24; 22:39), zile Heri (Mathayo 5:3–12), kuweka mbele ustawi wa kiroho kuliko ustawi wa mali (1 Timotheo 6:17–18), na kuzingatia kanisa (1 Petro 4:8; 1 Yohana 4:7; 2 Timotheo 2:22). Kuadhibu katika maeneo haya si fimbo na maonyo tu, bali ni kukuza kujizuia, kukuza hekima, kutafuta fursa za huduma, kuhimiza kuthubutu kufanya jambo, kufariji katika upinzani, kurekebisha unapotoshwa, na kutoa pumziko. Katika mafunzo ya wale Kumi na Wawili, Yesu alijumuisha kila moja ya haya kama kipengele cha mpango wake. Haikuwa saizi moja kuwatosha wote. Badala yake, ilihusisha kujali hali na mazingira ya uwezo, mwelekeo wa dhambi, ahadi, na uongofu wa wale aliokuwa akiwafundisha njia wanayopaswa kwenda.

Huko ni kutaka makubwa kutoka kwa wazazi. Kwa uhalisia, ni zaidi ya kile wanachoweza kufanya wao wenyewe. Lakini Mungu amewapa kwa neema kile wanachokosa katika kanisa lake. Ufuasi wa familia kwa ujumla unamaanisha kuwa na mtazamo wa kanisa ambao unaupa kipaumbele njia za kawaida za neema: Neno lililohubiriwa, sala, na sakramenti (pamoja na nidhamu ya kanisa). Baba ambaye halipi kipaumbele kanisa kwa ajili ya nyumba yake anawanyima wale anaowalea Neno lenye kuleta uhai na nafasi iliyobarikiwa ya utakaso. Anafanya mzaha wa amri zote za “kila mmoja” za Agano Jipya katika barua kwa makanisa. Iwe anafanya hivyo kwa sababu ni mvivu sana au “mwenye hekima” sana, anapaswa kujua kwamba hana haki ya kutarajia baraka kwa ajili yake au familia yake kupitia kujitenga na wacha Mungu. Kwa chaguo lake, anazalisha kitu ambacho ki chini ya mfuasi wa Kristo, ambaye alipenda kanisa na akajitoa kwa ajili yake (Efe. 5:2, 25).

Bila shaka, hakuna kanisa lililo kamilifu, lakini baadhi ya makanisa ni bora kuliko mengine (Mch. 2–3). Shirika la mahali lililochaguliwa vizuri na ibada ya pamoja katika Siku ya Bwana hutoa ubatizo na Neno lililohubiriwa, pamoja na fursa nyingi za kumtumikia Mungu na jirani, kufa kwa nafsi, na kubadilisha vipaumbele. Kupitia elimu ya Kikristo, familia nzima itasikia ukweli kutoka kwa sauti za ziada zikisema, “Hii ndiyo njia, ifuate” (Isa. 30:21). Ushirika wa Jumapili huwasaidia wale wanaojaribu kutembea na Kristo katika ulimwengu huu kujisikia kidogo kupungua kwa hali ya uwazimu na kufanya uanafunzi kuonekana kawaida zaidi. Uanafunzi ulikuja kama amri ya pamoja, na inatimizwa vyema katika muktadha wa pamoja. Nidhamu ya kiroho ya maisha kanisani si sehemu pekee ya uanafunzi wa familia, lakini ni muhimu zaidi.

Makala haya ni sehemu ya mkusanyiko wa Misingi ya Ufuasi wa Kikristo.

Scotty Anderson
Scotty Anderson
Rev. Scotty Anderson is associate pastor for family ministry at Woodruff Road Presbyterian Church in Simpsonville, S.C.
Ufuasi katika Familia
16 April 2026

Hakuna maandiko ya Biblia yanayozungumzia ufuasi yanayostahili kupewa umakini zaidi kuliko Agizo Kuu. Agizo hilo, au amri, linatolewa kwa wanafunzi (Math. 28:16) ili kuwafanya wanafunzi (Math. 28:19–20). Na Yesu anatoa jinsi ya kufanya hivyo: ubatizo wa Kikristo na mafundisho ya kibiblia. Kabla ya mzazi kufanya chochote kumwadhibu mtoto, ni vyema azingatie mpango wa Kristo wa kufanya wanafunzi. Nidhamu ya Kristo lazima iwe tabia ya nyumba zetu. Hiyo hakika inahusisha kuwarudi watoto kwa namna tunavyofikiria mara nyingi (Mith. 13:24; 19:18; 22:15; 23:13–14; 29:15–17), lakini pia inahitaji mengi zaidi kutoka kwa wazazi.

Bila kusoma Mithali kwa makini katika muktadha wa Maandiko yote, tunaweza (na mara nyingi tunafanya) kuangukia katika nadharia ya tabia,mbinu ya kisaikolojia ya kidunia inayochukulia kujifunza kwa binadamu ni kama suala la kuzoea matokeo tu. Lakini Kristo anatufundisha kwamba sisi na watoto wetu ni zaidi ya hayo. Tuna mioyo, vituo vya kiroho vya uwepo wetu, ambako tabia zetu hutoka (Mith. 4:23; Math. 12:33–35; 15:10–20; Luka 6:43–45). Biblia pia inafundisha kwamba mioyo yetu inazaliwa katika uovu (Zab. 51:5; Rum. 5:12), hivyo basi washiriki wa familia—wazazi na watoto—hatimaye wanahitaji kutatuliwa matatizo yao kutoka ndani kwenda nje.