Sababu Inayotumika katika Kuhesabiwa haki.
23 Juni 2025
Je, Mageuzo Yameisha?
23 Juni 2025
Sababu Inayotumika katika Kuhesabiwa haki.
23 Juni 2025
Je, Mageuzo Yameisha?
23 Juni 2025

Kwa kuwa Mungu ni Mwenye Enzi, Binadamu Wako Huru Vipi?

xr:d:DAFXk0WDSFg:25,j:45162075609,t:23011320

Mungu yu uhuru zaidi; yaani, uhuru wake hauna mipaka. Yeye ni Mwenye Enzi Pingamizi la mara kwa mara juu ya ukuu Wake ni kwamba ikiwa kweli Mungu ni mwenye enzi, basi mwanadamu hawezi kuwa huru. Maandiko hutumia neno uhuru kuelezea hali yetu ya kibinadamu katika njia mbili tofauti: uhuru kutokana na kulazimishwa, ambapo mwanadamu yuko huru kufanya maamuzi bila kulazimishwa, na uhuru wa kimaadili, ambao tuliupoteza katika anguko, ukatuacha watumwa wa mihemko mibaya ya miili yetu. Wafuasi wa itikadi ya ubinadamu (Humanists) wanaamini kwamba mwanadamu anaweza kufanya maamuzi siyo tu bila kulazimishwa bali pia bila mwelekeo wowote wa kiasili ya uovu. Sisi Wakristo lazima tuwe macho dhidi ya mtazamo huu wa kibinadamu au kipagani wa uhuru wa binadamu.

Mtazamo wa Kikristo ni kwamba Mungu hutuumba na nia, na uwezo wa kuchagua. Sisi ni viumbe wenye hiari. Lakini uhuru uliotolewa katika uumbaji una mipaka. Kinacho weka mipaka kwenye uhuru wetu hatimaye ni uhuru wa Mungu. Hapa ndipo kuna mgongano kati ya enzi kuu ya kiungu na uhuru wa binadamu. Wengine wanasema kwamba enzi kuu ya Mungu kikomo chake ni uhuru wa binadamu. Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo, basi mwanadamu ndiye mwenye ukuu, si Mungu. Imani ya Mageuzo inafundisha kwamba uhuru wa binadamu ni halisi lakini umewekewa mipaka na enzi kuu ya Mungu. Hatuwezi kubatilisha maamuzi ya enzi ya Mungu na uhuru wetu, kwa sababu uhuru wa Mungu ni mkubwa kuliko wetu.

Mahusiano ya kifamilia ya kibinadamu yanatoa mfano. Wazazi wana mamlaka juu ya mtoto. Mtoto ana uhuru, lakini wazazi wanao zaidi. Uhuru wa mtoto haupunguzi uhuru wa wazazi kwa njia ambayo uhuru wa wazazi unapunguza uhuru wa mtoto. Tunapokuja kwenye sifa za Mungu, lazima tuelewe kwamba Mungu yuko huru kabisa.

Wakati tunaposema kwamba Mungu ni mwenye enzi, tunasema jambo kuhusu uhuru Wake, ingawa tunadhania kwamba enzi kuu inamaanisha jambo tofauti kabisa na uhuru. Mungu ni kiumbe mwenye hiari; Ana nia na hufanya maamuzi. Anakufanya maamuzi na kutekeleza mapenzi Yake, Yeye hufanya hivyo kwa uhuru kama mwenye mamlaka ya juu kabisa. Uhuru wake ni huru zaidi. Yeye peke yake ana uhuru mkuu; Yeye ni sheria, Yeye Mwenyewe.

Binadamu wanatafuta uhuru, uhuru usio na mipaka, wakitamani kutowajibika kwa yeyote. Kwa kweli, hilo ndilo lililotokea katika anguko. Shetani aliwashawishi Adamu na Hawa kutafuta uhuru, wawe kama Mungu, wafanye chochote walichotaka bila kuadhibiwa. Shetani alikuwa akianzisha harakati za ukombozi katika bustani ili kuwaondolea wanadamu hatia, ya kutowajibika kwa Mungu. Lakini Yeye pekee ndiye awezaye kujitawala.


Dondoo hili limechukuliwa kutoka kwa Truths We Confess na R.C. Sproul.

Makala haya yalichapishwa kwanza katika Blogu ya Huduma za Ligonier.

R.C. Sproul
R.C. Sproul
Dkt. R.C. Sproul alikuwa mwanzilishi wa Ligonier Ministries, mchungaji wa kwanza wa mahubiri na mafundisho katika Saint Andrew’s Chapel huko Sanford, Fla., rais wa kwanza wa Reformation Bible College, na mhariri mtendaji wa gazeti la Tabletalk. Kipindi chake cha redio, Renewing Your Mind, bado kinapeperushwa kila siku katika mamia ya stesheni za redio ulimwenguni na kinaweza kusikilizwa mtandaoni pia. Alikuwa mwandishi wa vitabu zaidi ya mia moja, vikiwemo The Holiness of God, na Everyone’s a Theologian. Alijulikana ulimwenguni kote kwa utetezi wake mahiri wa Kutokukosea kwa Maandiko na uhitaji wa watu wa Mungu kusimama na ukweli wa Neno lake.