Kanuni inayotuongoza:

Utakatifu wa Ukweli


Kanuni kuu inayoongoza huduma yetu ni utakatifu wa ukweli. Ijapo tunajaribu kuwashawishi, kuwahimiza, kuwatia moyo watu, tunakuwa waangalifu kuepuka kuwateka akili, kama kulazimisha hatia ya uongo, au kutia chumvi manufaa au mahitaji ya huduma. Kwa  hivyo tumejitolea kwa viwango vifuatavyo;

  • Hatutafanya “maombi ya dharura” hata kama kuna dharura ya kifedha.
  • Hatutawasumbua watu kwa kuomba michango au kuwauzia kwa shinikizo.
  • Hatutatumia mbinu ya kudanganya wateja au kubadilisha ofa katika mauzo.
  • Hatutadanganya katika kupunguza bei za bidhaa.
  • Hatutaahidi faida za uongo ambazo hatuwezi kuhakikisha.
  • Hatutakana malalamishi ya wanafunzi kuhusu bidhaa zenye kasoro.
  • Tutajitahidi kuzingatia mahitaji ya wanafunzi kuliko yetu.
  • Tutakuwa wenye adabu na wapole kwa wanafunzi wetu.
  • Tutashughulikia mara moja maangizo na michango.
  • Tutatumia pesa kulingana mipangilio yake.
  • Tutatumia pesa zilizochangiwa mradi fulani kwa mradi huo tu.

Kama wasimamizi lazima tutoe hesabu kwa Bwana, ni lengo letu kukuza kanuni hizi za mwenendo katika wafanyikazi wetu:

Mtazamo wa huduma

  • Kuelewa na kuzidi matarajio ya washirika wetu.
  • Kuendeleza mazao ya kibiblia ya kweli na huduma za kuboresha maisha ya watu duniani kote.
  • Kutoa uongozi kitaalamu na maendeleo ya kibinafsi yakiongozwa na Neno la Mungu.

Shauku ya Uadilifu

  • Kukubaliana na viwango vya kanuni na mahitaji.
  • Tukijitahidi kufikia ubora kwa kuendelea kufafanua na kuboresha sehemu zote za huduma na uzalishaji.
  • Kukuza mahusiano yanayowafaidi wote kupitia uwazi, uaminifu, na kutengemewa.

Urithi wa Uaminifu

  • Kuiweka taasisi katika msimamo wa kutokosea kwa Maandiko na usahihi wa mafundisho.
  • Kutoa bidhaa na huduma kulingana na huduma ya maisha yote ya Dkt. Sproul.
  • Kuhakikisha kunausimamizi mzuri wa rasilimali.