
Kwa nini Mageuzo Bado Yanamaana
3 Julai 2025
Siku ya Mageuzo ni nini?
10 Julai 2025Imani na maungamo ya Kiprotestanti

Mageuzo ya Kanisa yalikuwa ni mapambano kuhusu mambo muhimu ya imani. Kwanza na Luther, na kisha na mapokezi mengine ya Kiprotestanti, Wanamageuzo waliweka imani ya kibiblia dhidi ya mafundisho ya Kanisa Katoliki la Kirumi na mamlaka ya kipapa. Kuashiria Biblia kama chanzo pekee cha mafundisho, Waprotestanti hata hivyo walilazimika kuelezea ufahamu wao wa mafundisho ya kibiblia. Kwa maana hii, Maungamo ya Mageuzo yalikuwa ni matokeo ya kawaida ya kujitolea kwa Waprotestanti kwa Biblia.
Waprotestanti hawakuvumbua haja ya maungamo. Kwa karne nyingi, kanisa limekuwa likikiri imani katikati ya mikanganyiko au migogoro. Jukumu la imani au ungamo halikuwa kamwe kuchukua nafasi ya Maandiko, bali ni kutoa muhtasari wa ushuhuda wa kanisa kwa ukweli katika Maandiko dhidi ya makosa.
Mifano maarufu zaidi ya msukumo huu ni imani za kihistoria—kama vile Imani za Nikea na Wakalkedoni—zilizoandikwa kati ya karne ya tatu na ya tano. Imani hizi zilitokana na haja ile ile kama maungamo ya baadaye ya Kiprotestanti—yaani, haja ya kufafanua kile ambacho kanisa limeshikilia kuwa ni muhimu katika masuala ya mafundisho.
Kilichotofauti kuhusu maungamo ya Kiprotestanti, hata hivyo, ni hamu ya Wanamageuzi kufanya mageuzo ya kina na ya kimsingi. Masuala ya Mageuzo hayakuwa tu mabishano juu ya fundisho moja—au seti moja ya mafundisho—bali yalitokana na haja ya kulirekebisha kanisa kabisa. Baadhi ya mafundisho, kama ya Utatu, yalihifadhiwa kama ya kibiblia, wakati mengine, kama kuhesabiwa haki kwa imani pekee, yalihitaji ufafanuzi wa makini. Kwa ajili ya makanisa katika mapokezi yao, viongozi wa Kiprotestanti walijitahidi kuandika kwa lugha ya kawaida mawazo yanayoelezea kukubalika kwa mafundisho kama vile kuhesabiwa haki kwa imani pekee au kukataa mamlaka ya kipapa.
Kwa maana hii, maungamo ya Kiprotestanti ni sawa na imani za awali, isipokuwa kina cha mtazamo wao kimeelezwa zaidi. Kama imani, hazibadilishi Maandiko, wala haziwekwi sawa na Maandiko. Badala yake, ni ufafanuzi wa kile ambacho Waprotestanti wanakipata katika Maandiko.
MAUNGAMO YA KILUTHERI
Mfano wa kwanza wa mwelekeo huu katika Uprotestanti unapatikana wakati wa Mageuzo ya Luther ya awali. Baada ya kupambana kwa ajili ya kuhesabiwa haki kwa imani pekee kutoka 1517 hadi 1519, na kutangazwa kuwa mhalifu na mzushi katika Baraza la Worms (1521), Luther alijishughulisha mara moja na kuandika misingi ya ujumbe wake katika seti ya nyaraka za maungamo. Mbili zilikuwa za kanisa na moja ilikuwa kwa ajili ya utetezi wa ujumbe wa Luther kwa umma.
Katika visa viwili vya kwanza, Luther aliandika Katekisimu Kubwa na Ndogo mnamo 1529, ya kwanza kwa ajili ya kufundisha watu wazima na makasisi na ya pili kwa watoto au waongofu wapya. Pia aliandika Himizo la Ungamo mwaka huo huo ili kuhalalisha haja ya ungamo. Ingawa kanisa linategemea Maandiko pekee, Luther alidai, haja ya ungamo la pamoja ni muhimu.
Katekisimu hizi za awali pia zinaashiria moja ya sifa bainifu za ungamo: ni zana za uanafunzi, muhimu kwa maisha ya kanisa.
Ungamo la tatu lilikuwa Ungamo maarufu la Augsburg (1530), ambalo liliandaliwa na Martin Luther na Philip Melanchthon. Lengo lake halikuwa kutoa ungamo la pamoja kwa ajili ya Kanisa lote, bali lilikusudiwa kuwasilishwa mbele ya mfalme Charles V na wakuu wa Ulaya. Ilikuwa ni ujumbe wa utetezi wa imani ya Kilutheri, wenye sauti ya mapambano wakati mwingine, au angalau katika maana zake. Inafafanua kile ambacho Walutheri waliamini dhidi ya mashtaka yaliyotolewa dhidi yao na Wakatoliki wa Ujerumani.
Katekisimu na maungamo ya Kilutheri, basi, zinaunda mfano mdogo wa njia ambazo maungamo yalitumika katika enzi za mageuzo: moja kwa ajili ya maisha ya kanisa, nyingine kwa ajili ya mabishano ya umma dhidi ya madai ya uongo kuhusu imani ya Kiprotestanti; moja kwa kila muumini kanisani, nyingine kwa viongozi wake kufafanua kile wanachoshikilia kuwa mafundisho sahihi.
MAUNGAMO YA KIMAGEUZO KUONGEZEKA
Mapokeo ya Mageuzo yalikuwa yamejitolea kwa usawa katika harakati za maungamo. Kulingana na mapana tutakayorusha wavu, kulikuwa na takriban maungamo arobaini hadi hamsini ya Mageuzo (au yaliyoathiriwa na Mageuzo)maungamo yaliyoandikwa kati ya 1520 na 1650—na ni zaidi ya utamaduni wowote wa Kiprotestanti. Mnamo mwaka wa 1523, mara tu baada ya kuanza kwa mapokeo ya Mageuzo, Huldrych Zwingli aliandika Makala Sitini na Saba ili kutoa ufafanuzi wa hoja zilizokuwa zinajadiliwa huko Zurich. Hii ilifuatiwa na Nadharia Kumi za Berne (1528), Ungamo la Kwanza la Basel (1534), na mengine kadhaa wakati miji ilipoanza kukubali mtazamo wa Mageuzo. Wengine wangefuata katika nchi nyingine, na Ungamo la Imani la Kifaransa (1559) na Ungamo la Uskochi (1560).
Sababu ya kuwepo kwa maungamo mengi ya Mageuzo yalitokana na miktadha yao. Imani ya Mageuzo daima iliongozwa na kundi la ndugu (licha ya mtazamo wa kisasa kwamba John Calvin pekee ndiye aliyeunda imani ya Mageuzo). Lakini mapokeo ya Mageuzo yalizaliwa katika miji na nchi kadhaa kwa karibu wakati mmoja. Kuanzia mwaka 1520 na kuendelea, mji baada ya mji ulikumbatia Mageuzo, mara nyingi hatua kwa hatua, na miji michache hata kabla ya mageuzo kufika Geneva. Kwa hiyo, hakukuwa na sauti moja kama ya Luther ya kuunda nyaraka za kimsingi za maungamo ya Mageuzo.
Matokeo yake, kanisa baada ya kanisa, jamii baada ya jamii zlitumia sehemu kubwa ya nguvu zao kuandika maungamo kwa makanisa yao. Hii ndiyo sababu maungamo mengi ya Kimageuzo yanajitambulisha na mji kwa asili yao: hili lilikuwa ungamo la mji huu, kanisa hili, si kwa makanisa yote ya Kimageuzo kuyakumbatia kama moja.
Hata hivyo, kama wanahistoria na wanatheolojia wanavyoeleza, kuna kuoanisha maungamo haya ya Mageuzo ambayo yanaunganisha sauti zao mbalimbali kuwa sauti moja ya Kimageuzo. Tofauti zao siyo kubwa sana kiasi kwamba hatuwezi kuona umoja wao katika masuala ya wokovu, ibada, na utendaji. Leo, makanisa mengi yanatambua maelewano ya kimsingi ya kile kinachoitwa Aina Tatu za Umoja—Ungamo la Kibelgiji, Kanuni za Dort, na Katekisimu ya Heidelberg—umoja si wa uandishi bali wa ushuhuda kwa kanuni za Kimageuzo.
Hii siyo kusema kwamba maungamo yote ya Kimageuzo yanafanana. Imani ya Kimageuzo iliposambaa kutoka kwa majimbo ya Uswisi hadi Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi, na kisha Uingereza na Uskoti, kulikuwa na tofauti za wazi za msisitizo au matumizi. Vitambulisho hivi vya kimaungamo vilitengeneza hatua za awali ambazo zingesababisha utofauti wa madhehebu ya Kimageuzo na jamii kama tunavyozijua leo.
WAPINGA U-KALVINI NA SINODI YA DORT
Nchini Uholanzi, kwa mfano, kuibuka kwa Uarminiani ndani ya makanisa ya Kimageuzo kulitoa muktadha wa Sinodi ya Dort (1618–19), matumizi ya kipekee ya kanuni za Kimageuzo kwa changamoto za Jacob Arminius. Baada ya kusoma huko Geneva chini ya mrithi wa Calvin, Theodore Beza, Arminius alirudi Uholanzi kuhudumu kama mchungaji. (Mojawapo ya kejeli kubwa ni kwamba Beza aliandika barua ya mapendekezo kwa Arminius aliporudi nyumbani.) Hata hivyo, Arminius, alizidi kuwa na shaka kuhusu elimu ya kidini ya Kimageuzo na mafundisho yake juu ya maamuzi ya kiungu ya awali na neema. Kwa muda, mafundisho yake yakawa mwito wa viongozi wengine kadhaa dhidi ya kuanzishwa kwa Ukalvini.
Baada ya kifo cha Arminius mwaka 1609, msimamo wa Arminian—pia unajulikana kama Imani yenye kupinga—iliorodhesha haraka hoja tano ambazo ziliwasilishwa kwa viongozi wa vita vya Uholanzi ili kujitenga na maeneo ya Kikatoliki yaliyodhibitiwa na Wahispania katika Uholanzi. Sinodi ya Dort ilikutana kujibu hili na ikakataa kila moja ya hoja hizo tano . Hivyo ndivyo zilivyozaliwa zinachojulikana kama hoja tano za Ukalvini, ingawa nia ya sinodi haikuwa kupunguza imani hadi hoja hizo tano, bali ilikuwa tu kutoa majibu kwa hoja tano za Uarminia.
Tukisonga mbele hadi mwishoni mwa karne ya kumi na saba, tunayaona maelezo haya ya mtu binafsi ya kanuni za Kimageuzo katika Ungamo la Imani la Baptisti la London (1689). Kama kule kuundwa kwa Wabaptisti wa Kipuritani—au Wabaptisti wa Kiasili (Primitive Baptists)—ungamo hili liliandikwa na wale waliokuwa wamejitolea kwa mafundisho ya Kimageuzo, ingawa walitofautiana na Wapresibiteri, Waanglikana, na Wakalvini wa Kiholanzi kuhusu mfumo wa uongozi wa kanisa (polity) na walikataa ubatizo wa watoto wachanga Ungamo hili lilikuwa kilele cha vizazi vya Wabaptisti vilivyoibuka nchini Uingereza na ambavyo vingekuja kufafanua mitazamo ya Wabaptisti wa Mageuzo kwa karne nyingi.
VIWANGO VYA WESTMINSTER
Alama ya juu ya ungamo, hata hivyo, ilikuwa Viwango vya Westminster, ambavyo vinajumuisha Ungamo la Imani la Westminster, Katekisimu Kubwa na Ndogo, Mwongozo wa Ibada ya umma(hadhara), na Mfumo wa Utawala wa Kanisa. Ungamo hilo lilikuwa maelezo mapya ya mafundisho sahihi ya Kimageuzo, huku katekisimu hizo mbili zikiiga dhamira ya Luther ya kutoa mwongozo wa imani kwa makasisi au watu wazima (Katekisimu Kubwa) na kwa watoto (Katekisimu Ndogo). Kwa upande wa urefu na kina, hakuna kiwango cha maungamo ya Mageuzo au baada ya Mageuzo kinacholingana na kile cha Mkutano wa Westminster. Historia yake, hata hivyo, inatokana na mapambano juu ya Upuritani ndani ya kanisa la Kiingereza.
Tangu wakati wa Henry VIII (aliyetawala 1509–47), kanisa la Kiingereza lilikuwa limekumbatia tu ungamo muhimu—kwanza Makala Arobaini na Mbili (1552), baadaye kupunguzwa hadi Makala Thelathini na Tisa (1563). Ingawa makala haya yalikuwa ya Kiprotestanti kikamilifu katika theolojia, hayakufafanua kujitolea kwa kanisa kwa kanuni za ibada na hayakubainisha msimamo juu ya mafundisho yenye utata kama vile miundo ya uongozi wa kikanisa au uwepo wa Kristo katika ushirika. Sehemu kubwa ya kushindwa kwa kanisa la Kiingereza kuandika ungamo kamili zaidi haikutokana na kusita bali kwa kutoweza kuliko sababishwa na mabadiliko makali kati ya uaminifu wa Kiprotestanti na Kikatoliki chini ya watoto wawili wa Henry, Edward VI na Mary I. Kwa sehemu kubwa ya karne ya kumi na sita, Kanisa la Kianglikana halikuwa na nafasi ya kuandika ungamo refu na lililo na umoja.
Wakati wa Elizabeth I, si wachache nchini Uingereza waliamini kuwa haja ya awali ya kuungama kwa kiasi kulikuwa ni fadhila. Maungamo mafupi yanaweza kupunguza idadi ya mabishano ya kidini ambayo yalikuwa yakijitokeza, kwa mfano, baina ya viongozi wa Mageuzo na wa Kilutheri barani Ulaya. Maaskofu kama vile Matthew Parker—ingawa walikuwa wamejitolea kwa imani ya Mageuzo—walianza kuonyesha wasiwasi juu ya sauti inayoongezeka ya kanisa la Kiingereza kubadilisha msimamo wake kuhusu ibada, mavazi, mafundisho, na desturi nyingine za liturujia.
Matokeo ya mvutano huu yalichochea kuibuka kwa Upuritani, kwanza chini ya Elizabeth na kisha kwa kiasi kikubwa chini ya James I. Jina hilo lilitumika kwa msukumo wa kutafuta mageuzo zaidi badala ya harakati iliyoelezwa waziwazi. hata hivyo Wapuritani wote walishiriki katika fadhaiko la kusitasita kwa maaskofu na viongozi wa kisiasa katika kuendeleza Mageuzo zaidi ya kanisa la Kiingereza.
Wakati wa Charles I, hali ilikuwa mbaya kiasi. Wakati wa utawala wa Elizabeth na James, Wapuritani mara nyingi walipuuzwa, ingawa kwa hakika hawakuteswa. Charles, hata hivyo, alionyesha msimamo mkali zaidi dhidi ya Wapuritani. Mwishoni, ugomvi kati ya Bunge na mfalme ulisababisha Vita vya Ndani vya Uingereza (1642–51).
Wapuritani walishinda mapambano, wakiongozwa na juhudi za kishujaa za Oliver Cromwell—ambaye sanamu yake hata leo hii bado ipo imara mbele ya Bunge. Wakati wa vita, Bunge liliamuru viongozi wa Kipuritani (na washauri wachache kutoka Uskoti) kuitisha mkutano ili kupanua Makala Thelathini na Tisa kuwa ungamo kamili lililolingana na maungamo mengine barani Ulaya. Bunge la Westminster lilifanya juhudi ya dhati za kuweka msingi wa kazi zao juu ya Makala Thelathini na Tisa, lakini punde waligundua kuwa mfano huu ulikuwa unabana sana, na hivyo wakaanza upya.
Muktadha huu wa mapambano dhidi ya Charles na haja ya Mageuzo zaidi unaeleza kwa urefu na kina Viwango vya Westminster. Badala ya kuonekana kama jaribio la kufupisha mafundisho yote, Viwango hivyo vinapaswa kuonekana kama mlipuko wa nguvu uliokuwa umejikusanya ndani ya Upuritani kwa ajili ya kufafanua mageuzo ya mafundisho na Imani ya Kiingereza. Damu ilikuwa imemwagika na sauti zimezimwa, na sasa kwamba sauti hizo zimeachiliwa kutoka kwenye vizuizi vyao, walihisi ni wajibu wao kueleza si tu msimamo wao wa kidini bali pia kuhusu ibada, ufuasi, na masuala mengine mengi katika maisha ya kanisa.
MAUNGAMO LEO
Leo, maungamo hutumiwa kwa njia mbalimbali katika maisha ya makanisa ya Kiprotestanti. Sio mitindo yote katika makanisa ya kiinjili inayokaribisha maungamo. Nguvu kama vile kuibuka kwa Uungu na Uamsho wa Pili Mkuu zimekuwa na athari ya kudhoofisha jukumu la maungamo—ya pamoja na ya kibinafsi—kwa kupendelea maelezo ya imani ya papo kwa papo. Wakati mwingine, maungamo yanaonekana kama vizuizi vya imani ya kweli.
Wakati ambapo mitindo hii inashtua, maungamo ya karne ya kumi na sita na kumi na saba hayajapita. Hutumiwa kila wiki katika makanisa mengi, katika muktadha wa ibada na katika katekismo za waumini wapya na watoto. Pia hutumiwa kuthibitisha uaminifu wa wachungaji na wazee katika madhehebu mbalimbali. Kwa maana hii, maungamo ya imani si tu yanaunda uzio wa mpaka unaosaidia kuhakikisha usahihi wa imani bali pia hutumika kama nyaraka hai zinazochora mwendo wa kila siku wa wanafunzi wa Kikristo.
Makala haya yalichapishwa kwanza katika Blogu ya Huduma za Ligonier.