Mambo Matano Unayopaswa Kujua Kuhusu Kuwa Mzazi
12 Agosti 2025
Mambo Matano Unayopaswa Kujua Kuhusu Kuwa Mzazi
12 Agosti 2025

Mambo Matano Unayopaswa Kujua Kuhusu Kuwa Mzazi

Kwa mengi yaliyosemwa kuhusu ndoa, ni muhimu kukumbuka mambo ya msingi. Iwapo umeingia katika ndoa au la, haya ndiyo mambo matano unayopaswa kujua kuhusu ndoa, yaliyofupishwa kwa maswali matano maarufu: nani, nini, lini, wapi, na kwa nini.

1. Nani: Ndoa imeundwa na Mungu, kwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja, walioungamanishwa sawasawa (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:4–5).

Mungu aliumba ndoa. Ikiwa tunatarajia baraka za Mungu juu ya ndoa, ni busara kufuata sheria Zake kuhusu ndoa. Muhimu zaidi kwa Wakristo, hii inamaanisha kushiriki imani sawa (2 Wakorintho 6:14). Wakati mwingine Mkristo hujikuta katika ndoa na mtu asiye Mkristo kwa sababu watu hubadilika. Pengine mwenza mmoja aingie katika imani au mmoja wa mwenza athibitishe kwamba hakuwahi kuwa na imani ya kweli tangu hapo awali. Ingawa Mungu anaruhusu ndoa za imani mchanganyiko, na hata kufanya kazi kupitia ndoa hizo, Anatuamuru sisi kutokuingia katika ndoa kama hiyo kwa chaguo letu. Kwa Mkristo kuchagua kuoa au kuolewa na mtu asiye Mkristo ni kwenda kinyume na Kristo badala ya kumkaribia, pia ni kupoteza mwendo na Roho badala ya kuandamana naye (Wagalatia 5:16–19).

2. Nini: Ndoa ni muungano wa maisha kati ya mume na mke, unaoonyesha uhusiano kati ya Kristo na kanisa.

Ndoa inahusisha watu wawili kuacha familia zao za asili ili kuanzisha familia mpya. Ndoa ya Kikristo ni picha ya uhusiano kati ya Kristo na kanisa, bibi arusi wake (Waefeso 5:32; 2 Wakorintho 11:2). Kwa hivyo, waume wanapewa amri zinazofanana na jukumu la Kristo kama kichwa cha kanisa. Waume wanaitwa kuongoza kwa kujitolea, hata kutoa sadaka maisha yao kwa ajili ya wake zao kama Kristo alivyofanya kwa kanisa (Waefeso 5:25). Vivyo hivyo, wake wanapewa amri zinazolingana na jukumu la kanisa kama mwili wa Kristo. Wake wanaitwa kuwatii waume zao kama kanisa linavyomtii Kristo (Waefeso 5:24). Majukumu yote mawili yana umuhimu sawia. Ni heshima na jukumu kubwa jinsi gani kwamba wanandoa wanapaswa kufunua uhusiano kati ya Kristo na kanisa kupitia ndoa zao.

3. Lini (wakati): Ndoa ni ya maisha, lakini si ya milele (Mathayo 22:30).

Ndoa ni kwa ajili ya maisha ya sasa hapa duniani, kama viapo vingi vinavyosema, “Kwa mema, kwa mabaya, kwa utajiri, kwa umaskini, katika ugonjwa na katika afya, mradi tu mtaishi wote wawili.” Sio tu kwa nyakati tunapohisi kupendwa au tunapohisi kupenda—ni ya maisha. Ingawa Mungu anatoa talaka kama chaguo katika hali maalum, haipaswi kufuatwa kama jibu kwa kila hali isiyotakiwa, isiyotarajiwa, au isiyo ya haki. Kwa kutarajia changamoto za ndoa, wanandoa huomba Mungu kwa busara ili aifanye upya, aiongeze, na hata kuzidisha upendo wao kwa kila mmoja (Mathayo 7:7), wakijua kwamba Mungu anafurahia kujibu maombi kama hayo (1 Yohana 5:14–15).

Sababu moja kwa nini wanandoa wanahitaji maombi kama haya ni kwa sababu bado sisi ni wenye dhambi, lakini hii si sababu ya kupoteza tumaini. Kufuata ule mfano uliowekwa na Kristo, Roho hutuwezesha kupendana kwa kujitolea. Uwepo wa dhambi si kikwazo kwa ndoa, bali ni mazingira yake tu. Mungu anawaita wanandoa, kwa neema Yake, kuvumiliana katika upendo (Waefeso 4:2). Wanandoa wenye busara humtumaini Mungu kuwasaidia kufanikisha ndoa isiyo kamilifu—na kutambua na kumshukuru Mungu kwa baraka zake nyingi ndani yake (1 Wathesaonike 5:18).

Iwapo upo ndani ya ndoa katika maisha haya au la, waumini wote kwa hakika watafurahia kikamilifu karamu ya harusi ya Mwana kondoo, ndoa moja ya kudumu na kamilifu kati ya Kristo na kanisa mbinguni kwa umilele wote (Ufunuo 19:6–9).

4. Wapi: Ndoa huanzisha familia mpya na nyumba mpya.

Kama Toleo la King James linavyosema kwa njia ya kishairi, Mungu anawaita mume na mke “kuacha na kushikamana” (Mwanzo 2:24). Kubadilisha uaminifu wa msingi kutoka kwa wazazi hadi kwa mwenzi kunaweza kuwa na changamoto. Kujitenga kati ya wanandoa na wazazi wao kunaweza kusaidia mchakato huu. Mungu anawaita wanandoa kuendelea kuwaheshimu wazazi lakini si lazima kuwatii (Kutoka 20:12; Waefeso 6:2–3). Wanandoa lazima watambue tofauti hiyo. Wanaweza kusikiliza ushauri wa wazazi, hata kukaribisha hekima yao, lakini wanandoa lazima wafanye maamuzi yao wenyewe kama familia iliyo huru, kwani ndivyo Mungu anavyowaona (Mwanzo 2:24).

5. Kwa nini: Mungu anatoa makusudi manne ya ndoa. Wanandoa wana muheshimu Mungu kwa kutafuta kutimiza yote manne kwa kadiri anavyowapa fursa.

  1. Kulea watoto. Wakati baadhi ya wanandoa wanaweza kuzuiwa kwa njia ya kimungu kupata watoto, Maandiko yanaona watoto kama baraka inayopaswa kutafutwa (Zaburi 127:3–5; Malaki 2:15), na wazazi wanapaswa kuwalea watoto katika nidhamu na mafundisho ya Bwana (Efeso 6:4).
  2. Kuridhishana kimapenzi. Mungu haruhusu ngono nje ya ndoa (1 Wakorintho 7:2). Ndani ya ndoa, inapaswa kufurahiwa, kama zawadi nyingine nzuri kutoka kwa Mungu.
  3. Kubariki dunia na kanisa. Mara nyingi, wanandoa ni zaidi ya jumla ya sehemu zake. Wawili wanaweza kuhudumu vizuri zaidi kuliko mmoja (Mhubiri 4:9–12, Mathayo 20:28).
  4. Urafiki. Wakati wa uumbaji, Mungu alipoumba kila kitu, alitangaza kuwa ni vyema (Mwanzo 1:31). Hali hiyo hiyo inaweza kusemwa kuhusu ndoa. Jambo moja ambalo Mungu alisema halikuwa jema ni kwa mwanadamu kuwa peke yake (Mwanzo 2:18).

Ikiwa kuna hoja moja ya kukumbuka, ni hii: ndoa ni nzuri. Ndoa ni njia moja muhimu ambayo Mungu hutumia kuwapatia watu wenza wa maisha, na tunafanya vyema kutarajia baraka zake nyingi juu yake tunapomheshimu ndani yake.Makala hii ni sehemu ya mkusanyiko wa Mambo Matano Unayopaswa Kuyajua.


Makala haya yalichapishwa kwanza katika Blogu ya Huduma za Ligonier.

Emily Van Dixhoorn
Emily Van Dixhoorn
Emily Van Dixhoorn alihitimu kutoka Seminari ya Theolojia ya Westminster. Yeye ni mwandishi mwenza wa kitabu cha Gospel-Shaped Marriage: Grace for Sinners to Love Like Saints na mwandishi wa Confessing the Faith Study Guide. Emily na mume wake Chad wanaishi Charlotte, NC na Watoto wao watano.