
Injili Inamaanisha Nini?
23 Juni 2025
Martin Luther Alikufaje?
30 Juni 2025Kwa Nini Unafanya Kazi?

Kwa nini unafanya kazi? Wakati mmoja nilisikia jibu la kusikitisha ambalo lilikwenda hivi: “Tunapata kazi ili tuweze kuwanunulia watoto wetu viatu, ili waweze kwenda shule, ili waweze kupata kazi siku moja, ili waweze kununulia watoto wao viatu, ili wao . . .” Kwa maneno mengine, kazi haina maana. Kwa kweli, kutoka kwa mtazamo huu maisha yenyewe yanakuwa hayana maana—ni mzunguko usio na mwisho.
Nimesikia pia ikisemwa kwamba tunafanya kazi ili tuweze kusaidia huduma zinazofanya kazi halisi—kazi ya ufalme. Sasa, sipingi kutoa kwa huduma za kidini. Kwa kweli, nadhani unaweza kutoa hoja yenye nguvu ya kibiblia kwamba tunalazimika kufanya hivyo. Lakini ninashangaa kama hii inaonyesha kikamilifu maana ya kazi.
Kwa hiyo tena, kwa nini unafanya kazi? Ninapata mwanzo wa jibu hili katika Zaburi 104. Zaburi 104 ni tafakari juu ya uumbaji na labda hata tafakari zaidi juu ya gharika ya Mwanzo 6–8. Tunaona mtunga zaburi akielezea kwa kishairi sio tu uumbaji wa Mungu wa dunia na viumbe vyote, bali pia tunaona kazi ya karibu ya Mungu katika kudumisha uumbaji Wake na viumbe alivyoviumba (vf. 1–13).
Katika kifungu cha 14, tunasoma kwamba Mungu anatoa kwa ajili ya mifugo na watu pia. Lakini pia tunasoma kwamba watu wana jukumu. Wao wanapaswa kulima mimea ambayo Mungu husababisha ikue. Kile tulicho nacho hapa ni kazi ya kubeba picha katika vitendo. Kama wale ambao wameumbwa kwa sura ya Mungu, tunapaswa kuwa na utawala na kuitiisha dunia. Nituipanua bustani hiyo ya asili, tuliyopewa na Mungu. Tunaona hapa matumizi ya agizo la kitamaduni la Mwanzo 1:26–28.
Tunaona hili katika vifungu vya 21–23 vya Zaburi 104 pia. Kama vile simba wanavyotoka kutafuta mawindo—wanavyofanya kazi kama walivyoumbwa—Kisha mwanadamu ”huenda kazini mwake,katika kazi yake mpaka jioni.” (v. 23). Kuna mshikamano hapa ambao haupaswi kupuuzwa. Viumbe wote wa Mungu, wakubwa kwa wadogo, wanawasilishwa kama wanaofanya kazi kwa ushirikiano na muundo wao wa asili, walioumbiwa. Simba waliumbwa kufanya kazi kama simba. Tuliumbwa kufanya kazi kama wale waliochukua sura ya Mungu. Kwa kweli, mwandishi wa zaburi anaenda kwa urahisi si tu kutoka kiumbe hadi kiumbe kingine, bali pia kutoka kwa viumbe hadi kwa Mungu, Muumbaji. Katika kifungu kinachofuata, kifungu cha 24, Mwandishi wa Zaburi anatangaza, “Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote,dunia imejaa viumbe vyako.”
Mwandishi wa zaburi anataka tuhusishe kazi zetu na masuala yenye maana ya kina na mapana zaidi. Tunapofanya kazi, ni picha ya kazi ya Mungu, Muumbaji. Katika kazi yetu ya kutawala na kuwa na mamlaka, katika kazi yetu ya kulima, tunaona kitu kingine. Kazi yetu inatoa ushuhuda na inaashiria yule ambaye kwa mfano wake tumeumbwa. Kazi yetu ni ushuhuda, ikiashiria, kwa Mungu Muumba. C.S. Lewis aliwahi kusema kwamba hatujawahi kukutana na mtu wa kawaida. Labda tunaweza kusema kwa maneno mengine: Hatufanyi kazi ya kawaida kamwe. Kazi si ya kijinga, isiyo na maana, isiyo na lengo, ya kipuuzi, au isiyo na umuhimu. Kazi yetu inaeleweka vyema kama iliyojaa maana na umuhimu.
Lakini, subiri, kuna zaidi.
Katika vifungu vya 25–26, tunasoma:
Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele,
imejaa viumbe visivyo na idadi,
viumbe hai vidogo na vikubwa.
Huko meli huenda na kurudi,
pia Lewiathani,uliyemuumba acheze ndani yake.
Ni wazi kwamba bahari na viumbe wa baharini wanashuhudia ukuu, utukufu, na uzuri wa Mungu Lakini angalia kwa makini kifungui cha 26. Mwandishi wa zaburi anaweka vitu viwili sambamba: meli na Leviathani. Vitabu vya kishairi, kama Zaburi na Ayubu, na hata kitabu cha kinabii mara kwa mara, vinarejelea kiumbe hiki.
Lewiathan. Hakujakuwa na uhaba wa uvumi kuhusu utambulisho halisi wa kiumbe hiki. Je, ni nyangumi mkubwa? Je, ni dinosaria? Ngisi mkubwa? Tunachojua kwa hakika ni kwamba Lewiathan anatushangaza sana. Kunauwezekano wa kutumia neno kushangaza mara nyingi sana na kwa hivyo tumepunguza nguvu yake ya kisarufi. Lakini katika suala hili, neno hilo linafaa. Lewiathan ni wa ajabu.
Lewiathan pia anapenda kucheza. Hatuwezi kukosa hilo. Jonathan Edwards, katika kuandika kuhusu buibui anayepaa, anabainisha kwamba wakati buibui huyu alipopaa alikuwa na tabasamu usoni mwake. Hili lilimfanya Edwards kufikia uamuzi kwamba Mungu alitoa “kwa ajili ya furaha na burudani kwa viumbe wa aina zote, hata wadudu.” Hata Lewiathani. Mnyama huyu wa ajabu anacheza. Na kisha kuna kiumbe mwingine katika kifungu cha 26. Kiumbe hiki kimeundwa na binadamu: “Hapo zinakwenda meli.” Sasa, lazima tufikirie hili kwa makini. Uumbaji wa Mungu na uumbaji wetu unawekwa bega kwa bega, karibu karibu, sambamba. Mwandishi wa zaburi anashangazwa na Lewiathani, na mwandishi wa zaburi anashangazwa na meli. Unaweza kuwa na taswira hiyo. Labda umewahi kusema mwenyewe: “Tazama, meli hiyo inaelea. Ajabu.”
Nini hujumuishwa katika ujenzi wa meli? Hisabati na fizikia, useremala wenye ujuzi, uzoefu, utaalamu wa pamoja wa vizazi vingi kupitia majaribio na makosa mengi, kazi nyingi—yote haya yanaingia katika ujenzi wa meli. Nini kinaingia katika safari ya meli? Mbinu za uongozaji meli, utaalamu, misuli, migongo imara, mikono imara, ujasiri, azimio, hekima ya pamoja ya vizazi—yote haya yanaingia katika safari ya meli.
Mwandishi wetu wa zaburi anashangazwa anapoona meli zikivuka upana wa bahari. Mwandishi wetu wa zaburi anashangazwa anapomwona Lewiathani akicheza juu ya upana wa bahari. Hizi vya ajabu sana, kweli.
Tunagundua, tunapoendelea kusoma zaburi hii, kwamba kuna zaidi hapa kuliko majitu ya asili na ya kutengenezwa na binadamu kuvuka bahari na kucheza kwenye mawimbi. Kifungu cha 27 kinatuambia: “Hawa wote,” ikimaanisha viumbe vyote vya Mungu, “wanakutegemea wewe, kuwapa chakula chao kwa wakati unaofaa. . . .” Wakati unafungua mkono wako, wanajazwa na vitu vizuri.” Tunapata furaha, tunapata utimilifu, tunapata maana kutoka kwa kazi zetu. Tunatambua vipawa vyetu tulivyopewa na Mungu, rasilimali zetu tulizopewa na Mungu, kisha tunaanza kufanya kazi. Na kisha tunaridhika. Divai hufurahisha mioyo yetu (K. 15). Viumbe vyetu vinatustaajabisha.
Haya yote ni matokeo ya kazi yetu. Lakini hakuna hata moja kati ya haya ambalo ni lengo kuu au matokeo ya mwisho ya kazi yetu. Lengo kuu la kazi yetu linakuja katika kifungu cha 31: “Utukufu wa Bwana na udumu milele, Bwana na azifurahie kazi zake.” Kazi yetu ina maana. Kazi yetu inaashiria Yule ambaye kwa mfano wake tumeumbwa. Tunapofanya kazi, tunamletea Mungu utukufu. Tunapofanya kazi, Mungu hufurahishwa na sisi. Sasa tumepata jibu letu kwa nini tunafanya kazi.
Je, uliona nini hakipo katika Zaburi 104? Hakuna rejeleo hata moja kwa hekalu, kwa wanamuziki wa hekalu, kwa makuhani na shughuli zao. Kuna marejeleo ya kilimo. Kuna marejeleo ya kutunza mizabibu. Kuna marejeleo ya kazi za mikono. Kuna marejeleo ya kazi.
Kuna marejeo ya kujenga meli.
“Hapo ndipo meli zinapoelea” Utukufu kwa Mungu.
Makala haya yalichapishwa kwanza katika Blogu ya Huduma za Ligonier.